Waziri Mkuu Majaliwa atoa ufafanuzi kuhusu ongezeko la mshahara kwa wafanyakazi leo Julai 29, 2022

Waziri Mkuu Majaliwa atoa ufafanuzi kuhusu ongezeko la mshahara kwa wafanyakazi leo Julai 29, 2022

Mr Q

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
18,046
Reaction score
38,598
Sina mengi ni kuanzia saa kumi jioni. Japo wadau wengi hawana imani tena baada ya kupitia uzoefu fulanifulani zilizo tolewa ufafanuzi kupitia ofisi ya Waziri Mkuu.
===

Aliyoyazungumza waziri Mkuu.

Rais Samia Suluhu Hassan tangu ameingia madarakani amehakikisha watumishi wanapata amani mahali pa kazi. Na wakati wote amesisitiza kazi zenye matokeo chanya ili kuleta maendeleo kwenye taifa hili. Naliwaambia hatowaangusha alipokuwa akizungumza na watumishi Mwanza siku ya Wafanyakazi

Akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi amesema Rais ameahidi kuboresha maslahi ya watumishi ikiwemo kulipa madai. Ikiwemo madai ya kazi mbalimbali na madai ya kubadilika na kupanda madarajaambayo walipanda muda mrefu na ikatengeneza malimbikizo.

Amesema inawezekana kuna sekata haijalipwa lakini bado serikali inaendelea kuwalipa watumishi. Aliboresha maslahi ya watumishi kwa kutaka watumishi waliokaa muda mrefu bila kupandishwa madaraja wakapandishwa madaraja.

Pia Rais amesema suala la kodi liliangaliwa kutoka kwenye double digits hadi single digit ambayo ilifikia 9% ambapo Rais Samia aliishusha hadi 8% na inaweza kushushwa zaidi ili watumishi wapate maslahi zaidi

Serikali Imeajiri watu zaidi 44 elfu
Maslahi mengine yaliyoongezwa ni kubadilisha miundo ya kiutumishi ili kutengeneza nafasi ya wengine kuingia. Hadi sasa watu zaidi ya elfu 44 wameajiriwa na kati yao zaidi ya elfu 22 wameingiza kwenye payroll. Ajira hizo hazijumuishi ajira za sekta binafsi.

Waziri amesema unafuu mwingine uliopatikana ni suala la mikopo ya elimu ya elimu ya juu ambayo ilikuwa inakatwa mara tu mtu anapoanza ajira.

Asilimia ya ongezeko iliyotajwa iliwalenga watumishi wa kima cha chini. Na watu waliokuwa wanapata maapato makubwa hawapati asilimia iliyotajwa kwa kuwa ukiwalipa kwa asilimia ile mapato yao yatakuwa ya juu zaidi. Hivyo tumepandisha katika hali ambayo haifanyi ile tofauti isiwe kubwa.

Asilimia ya ongezeko iliyowekwa inaweza kuonekana haikidhi lakini kwa nia ya muheshimiwa Rais kuna matumaini hapo baadae ikafikia hatua nzuri.

SERIKALI: UPANDISHAJI MISHAHARA UNAANGALIA HALI YA UCHUMI

Akizungumza kuhusu Nyongeza ya Mishahara, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema katika mchakato ya upandishaji Mishahara, Serikali inaenda kwa kuangalia Hali ya Uchumi wa Nchi ili kutokwama katika mambo mengine

Amefafanua, "Tunaangalia gurudumu hili tunavyolipeleka sisi wenyewe tusije tukalikimbiza likatukwamisha, tukafika mahali tumegota tukashindwa kwenda. Mwenendo huu wa kiuchumi sisi ndio tunaushikilia, tunausimamia na tunautekeleza"

KUNDI KUBWA LIMENUFAIKA NA ONGEZEKO LA MISHAHARA
Waziri Mkuu amesema ongezeko lilifanywa kwa watumishi wa serikali limewanufaisha watumishi wengi ambao ni zaidi ya 75%. Watu wanaolalamikia ongezeko dogo ni wale wenye mishahara mikubwa kama mawaziri na wakurugenzi ambao wamepata hadi 0.7%.

23% haijatumika kwa watu wote kutokana na ile formula ya kuongeza mishahara.
 
Watumishi wa Umma hawana hamu kabisa ni hilo ongezeko uchwara
Kitu
Screenshot_20220729-153048.png
kizito
 
Sina mengi ni kuanzia saa kumi jioni. Japo wadau wengi hawana imani tena baada ya kupitia uzoefu fulanifulani zilizo tolewa ufafanuzi kupitia ofisi ya Waziri Mkuu.



Naambatanisha pichaView attachment 2308031

 
Katumwa kutupa moyo mgumu
 
Back
Top Bottom