Waziri Mkuu Majaliwa atoa ufafanuzi kuhusu ongezeko la mshahara kwa wafanyakazi leo Julai 29, 2022

Nimesema huyu Mzee NI mwongoooo amesomea propaganda
Siasa Kazi rahisi sana, unawadanganya watu wazima wenzako halafu basi.

Kinachotokea hapa ni kwamba serikali inataka kuwachongonisha watumishi na wananchi, ionekane watumishi wanadai mishahara mikubwa, Wana tamaa....hakukuwa na haja ya kufanya hii press, hakuna cha maana kilichozungumzwa zaidi ya kupigilia msumari wa Moto kwenye kidonda kibichi.

Ila kwenye propaganda na uchonganishi Kati ya watumishi na wananchi press inaweza kuwa na maana.
 
Maelezo yote aliyoyatoa watumishi (ambao ni wasomi) wanayajua,km alikua na speech hii ni kheri angekausha tu...
#Maendeleo Hayana Chama
 
Mawaziri na wakurugenzi mnawapandisha kwa 0.7% ambao sio mawaziri na wakurugenzi 0.4%
 
Kifupi waziri anasema kundi dogo linalopiga kelele limepewa 7% na kundi hili n mawaziri na mfanano wake huku kundi kubwa waalimu, watu wa afya, watu wa utawala wamepewa 23% na walalamiki hata kdg

Kwamba kundi dogo la mawaziri linataka 23% ndo alikuwa analijibu hahahaha hakuna waziri hapo
 
Katika Mei Mosi 2022, mama alishamaliza kuwa jambo letu lile lipo na watu walishaanza kutulia.....kutokana na kauli ile, hata ingeongezeka 1% hakuna ambaye angeshangaa wala kupjgapiga makelele. Nini tena kilisababisha serikali itamke kuwa kuna ongezeko la 23.3% wakati ilikuwa haijajiandaa vya kutosha kimaelezo na kivitendo ili kujiepukia vitu kama hivi ambavyo vinaleta migogoro isiyo ya ulazima na upotevu wa muda muhimu wa serikali km leo ambao ungetumika kufanya mambo mengine ya kimaendeleo ?!!!!!!!!!!!
 
Okey, hiyo 23% imeongezeka kwa watu waliokuwa wanapata mishahara midogo, ni vizuri, lakini pia muangalie namna ya kuweza kushusha gharama za maisha, mana gharama za maisha zimepanda kwa watu wenye mishahara yote na sio wa kima cha chini pekee, japo kuna changamoto za magonjwa na vita inayoathiri uchumi na kuwa changamoto, ila kw kadhri muwezavyo muweze kushusha gharama za maisha zinazopanda kwa kasi bila kudhibitika,otherwise all the best kwenye utendaji kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…