Waziri Mkuu Majaliwa awasilisha pongezi kwa Dkt. Tulia Ackson kwa utendaji wake katika Bunge la IPU

Waziri Mkuu Majaliwa awasilisha pongezi kwa Dkt. Tulia Ackson kwa utendaji wake katika Bunge la IPU

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa, imempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson, kwa Uongozi wake mahiri na ujasiri aliouonesha katika tukio lililotokea wakati wa Mkutano wa 149 wa IPU uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu mjini Geneva, Uswisi.

Majaliwa amesema “Watanzania tuna kila sababu ya kujivunia ushupavu aliouonesha wakati wa Mkutano huo na jinsi alivyodumisha msimamo thabiti wakati wote. Sina shaka kuwa Uongozi wake utaacha alama ya kudumu katika historia ya Umoja wa Mabunge Duniani.”

Aidha, Majaliwa amewaomba Wabunge na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Spika ili aweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

Soma Pia: Tulia Ackson kwenye Bunge la Dunia amejibu maswali vema sana. Ila ni vema adhibiti 'emotions'

“Sote kwa pamoja, tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu amjalie uzima, hekima na nguvu katika kuutumikia Umoja huo duniani,” amesisitiza Majaliwa.
 
Back
Top Bottom