Waziri Mkuu Majaliwa azuia magari ya Serikali kununulia nyanya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Maafisa Elimu na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanayatunza magari waliyokabidhiwa na serikali na kwamba atakayekutwa amepaki gari kisa kukosa 'service' atakuwa hana kazi na kwamba magari hayo yasitumike kununulia nyanya wala kwenda nayo bar.

PMMM.jpg
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Kauli hiyo ameitoa jana Mei 21, 2021, wakati akikabidhi jumla ya magari 184 yenye thamani ya shilingi bilioni 16.4, kwa maafisa elimu wa Halmashauri ikiwa ni mkakati wa serikali ya awamu ya sita kuendelea kuboresha sekta ya elimu nchini na kuzitaka Halmashauri zilizopokea magari hayo kuzingatia taratibu za serikali katika matumizi na matengenezo ya magari hayo.

"Magari haya mmekabidhiwa, maafisa elimu na wakurugenzi wa Halmashauri, tukute gari limepaki kisa limekosa ‘Service’ utakuwa umekosa kazi, lazima tuambizane ukweli, magari haya lazima yafanye kazi kwa zaidi ya miaka mitano hadi sita, na yatumike kwa ajili kufuatilia masuala ya elimu, haya siyo magari ya kwenda kununulia nyanya, wala kupumzika nayo Bar", alisema Waziri Mkuu

Amesema kuwa magari hayo ni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za ufuatiliaji na tathmini kwa Maafisa Elimu, na yametolewa na serikali ili yasaidie kuharakisha shughuli za utekelezaji wa majukumu katika sekta ya elimu.

eatv
 
Kwa hiyo tukiwa tunatoka safari zetu nyanya tuwe tunaziona kama kituo cha polisi....mambo gani haya, haya wacha nyanya ziwadodee wakulima maana tumeshakatazwa kununua nyanya....
 
Shule hazina vifaa unampa afisa elimu gari ya kufuatilia shule hizo!
Tena inabidi yawe magari ya juu (4 x 4) maana shule zenyewe zipo kwenye maeneo yenye barabara mbovu.
 
Sijayaona hayo magari lakini naamimi mengi ni TOYOTA LANDCRUISER HARDTOP AU TOYOTA HILUX,
Naamini pia kama sera zao zilivyo wananunua brand new cars toka kwa dealers.
TAFAKURI...Hivi LandCruiser au Hilux mpya unaiwekea makadirio ya kutumika sana sana eti olny 5 years au eti unaiwazia mbaaaaaaali basi miaka sita tu,kweli!!!!
Watu wana vi ist vyao na tuvits tuna miaka saba sasa na bado tunadunda vizuri tu barabarani.
WAZO.....Ifike hatua serikali iangalie upya makadirio ya muda wa matumizi kwa haya magari wanayonunua aysee,au basi haina haja ya kununua brand new cars tena kwa gharama kubwa kwa kiasi hiko kama approximation ya matumizi yake ni miaka hiyo sita au hata kumi.

Waje mitaani watuulize wananchi magari yetu tumeyanunua kwa bei gani na hadi muda huu yana umri gani bado yapo mikononi mwetu na bado yapo vizuri tu!!!!
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Maafisa Elimu na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanayatunza magari waliyokabidhiwa na serikali na kwamba atakayekutwa amepaki gari kisa kukosa 'service' atakuwa hana kazi na kwamba magari hayo yasitumike kununulia nyanya wala kwenda nayo bar.

PMMM.jpg

Kauli hiyo ameitoa jana Mei 21, 2021, wakati akikabidhi jumla ya magari 184 yenye thamani ya shilingi bilioni 16.4, kwa maafisa elimu wa Halmashauri ikiwa ni mkakati wa serikali ya awamu ya sita kuendelea kuboresha sekta ya elimu nchini na kuzitaka Halmashauri zilizopokea magari hayo kuzingatia taratibu za serikali katika matumizi na matengenezo ya magari hayo.

"Magari haya mmekabidhiwa, maafisa elimu na wakurugenzi wa Halmashauri, tukute gari limepaki kisa limekosa ‘Service’ utakuwa umekosa kazi, lazima tuambizane ukweli, magari haya lazima yafanye kazi kwa zaidi ya miaka mitano hadi sita, na yatumike kwa ajili kufuatilia masuala ya elimu, haya siyo magari ya kwenda kununulia nyanya, wala kupumzika nayo Bar", alisema Waziri Mkuu

Amesema kuwa magari hayo ni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za ufuatiliaji na tathmini kwa Maafisa Elimu, na yametolewa na serikali ili yasaidie kuharakisha shughuli za utekelezaji wa majukumu katika sekta ya elimu.

eatv
ila MA VXR yetu wanapaki Kibaigwa kununua nyanya na mikaa kule mdaula, haya endeleeni.
 
Serikali masikini, watuwake wana ishi ktk dimbwi la ufukara, kila kionhozi anataka anunuliwe V8 Magari yanayo filisi nchi na kuteketeza fedha za walipa kodi.

Tunaomba serikali yetu iweke mkazo wa kubana Matumizi ya fedha za umma ktk mambo mbalimbali mfano;

1. ununuzi wa magari kwa viongozi ukimuacha Rais, Makamu na waziri mkuu walio baki watumie magari kulingana na vyeo vyao. haya magari wanayo tumia sasa ni hataki kwa uchumi wetu.

2. safari za nje ya nchi kamwe zisiruhusiwe.

3. semina zisizo na tija.

n.k
 
Sijayaona hayo magari lakini naamimi mengi ni TOYOTA LANDCRUISER HARDTOP AU TOYOTA HILUX,
Naamini pia kama sera zao zilivyo wananunua brand new cars toka kwa dealers.
TAFAKURI...Hivi LandCruiser au Hilux mpya unaiwekea makadirio ya kutumika sana sana eti olny 5 years au eti unaiwazia mbaaaaaaali basi miaka sita tu,kweli!!!!
Watu wana vi ist vyao na tuvits tuna miaka saba sasa na bado tunadunda vizuri tu barabarani.
WAZO.....Ifike hatua serikali iangalie upya makadirio ya muda wa matumizi kwa haya magari wanayonunua aysee,au basi haina haja ya kununua brand new cars tena kwa gharama kubwa kwa kiasi hiko kama approximation ya matumizi yake ni miaka hiyo sita au hata kumi.

Waje mitaani watuulize wananchi magari yetu tumeyanunua kwa bei gani na hadi muda huu yana umri gani bado yapo mikononi mwetu na bado yapo vizuri tu!!!!

wewe unajua shughuri za ufuatiliaji na mazingira ambayo yanawakabili maifisa elimu..? Embu siku moja jaribu ww na Toyota IST yako kuifuta Toyota Land Cruiser semehu inazopita. Hoja yangu miaka mitano ni sawa tu kwa kuwa magari mengi ya serikali yanafanya kazi katika mazingira magumu, lakini pia huwa zinatumika ktk shughuri mbalimabali ambazo zinafanya haya magari kutumika sana. Tofauti na private cars.
 
Sijayaona hayo magari lakini naamimi mengi ni TOYOTA LANDCRUISER HARDTOP AU TOYOTA HILUX,
Naamini pia kama sera zao zilivyo wananunua brand new cars toka kwa dealers.
TAFAKURI...Hivi LandCruiser au Hilux mpya unaiwekea makadirio ya kutumika sana sana eti olny 5 years au eti unaiwazia mbaaaaaaali basi miaka sita tu,kweli!!!!
Watu wana vi ist vyao na tuvits tuna miaka saba sasa na bado tunadunda vizuri tu barabarani.
WAZO.....Ifike hatua serikali iangalie upya makadirio ya muda wa matumizi kwa haya magari wanayonunua aysee,au basi haina haja ya kununua brand new cars tena kwa gharama kubwa kwa kiasi hiko kama approximation ya matumizi yake ni miaka hiyo sita au hata kumi.

Waje mitaani watuulize wananchi magari yetu tumeyanunua kwa bei gani na hadi muda huu yana umri gani bado yapo mikononi mwetu na bado yapo vizuri tu!!!!
Hiyo mimi nikiinunua used kutoka huko kwa mjapenga kikiwa kimeshakata kilometa 70000+, naitumia zaidi ya miaka mi5 na chombo bado kinakuwa nyuu kabisa.

Ifike sehemu serikali iache masihara iheshimu pesa zetu, wana matumizi fulani ya kibwege bwege.. Sasa waziri anakataza wasibebee nyanya [emoji23], mtu atoke safarini aone nyanya bidhaa nzuri aache kununua, haiwezekani.
 
  • Thanks
Reactions: y-n

Maneno Yao Siyo Msahau
PM Ana Gari Tele Mpaka Kuhudumia Home Kwake
 
Back
Top Bottom