Mkuu,sijui unazizungumzia halmashauri za wapi mkuu,kokote nchini,kila kona ya nchi huwezi kukosa hizi gari ambazo hapa unazidharau,zipo hadi paso huko vijijini tena ndani kabisa,halafu unaposema matumizi ga gari za serikali ni tofauti sana kwani kuna matumizi gani tofauti na kutembea tu ?au unafiki gari ikitembea ndio inakufa?
Mkuu,unadhani hizo shule ambazo kiukweli kabisa hazifikiki kirahisi na miundombinu ni mibovu kabisa hao maafisa elimu wanaenda basi,au hata wakienda inafika hata mara moja kwa mwaka?
Mkuu inawezekana kuna vitu huvijui kabisa kuhusu haya magari,au unajua kiasi,au unajua ila upo katika macho yaliyofunikwa au umekariri tu.
Kwa mfano,ukimpatia afisa elimu TOYOTA KLUUGER ya 20M ni maeneo gani anaweza ashindwe kufika kabisa kisa hana usafiri?
Mchina ambaye ameweka madubu yake ameweka hadi vijiji vya ndani ndani huko kabisa na bado anayafuatilia zaidi ya mara moja kwa wiki na anatumia Kluger.
Mkuu,bado huamini kama hata manunuzi na matumizi ya hizo gari ni utumiaji mbovu wa pesa zetu?
LandCruiser sio chini ya 120M,mkuu,ukinunua Kluger moja na NISSAN X TRAIL MOJA ambazo hazizidi hata 40M ukampatia afisa elimu huyo huyo kwa matumizi ya miaka hiyo mitano hadi sita,je hayo magari hayatofika?
Hebu tuambiane UKWELI Kwanza mkuu