Waziri Mkuu Majaliwa azuia magari ya Serikali kununulia nyanya

Matumizi ya private car ni tofauti kabisa na hizi za serikali, hizi halmashauri wakifanya ufuatiliaji wa uhakika adi uko vijijini shule zilipo miaka 5 ni sawa kabisa
 
Matumizi ya private car ni tofauti kabisa na hizi za serikali, hizi halmashauri wakifanya ufuatiliaji wa uhakika adi uko vijijini shule zilipo miaka 5 ni sawa kabisa
Una masihara saana ndugu yangu.
 
Matumizi ya private car ni tofauti kabisa na hizi za serikali, hizi halmashauri wakifanya ufuatiliaji wa uhakika adi uko vijijini shule zilipo miaka 5 ni sawa kabisa
Mkuu,sijui unazizungumzia halmashauri za wapi mkuu,kokote nchini,kila kona ya nchi huwezi kukosa hizi gari ambazo hapa unazidharau,zipo hadi paso huko vijijini tena ndani kabisa,halafu unaposema matumizi ga gari za serikali ni tofauti sana kwani kuna matumizi gani tofauti na kutembea tu ?au unafiki gari ikitembea ndio inakufa?
Mkuu,unadhani hizo shule ambazo kiukweli kabisa hazifikiki kirahisi na miundombinu ni mibovu kabisa hao maafisa elimu wanaenda basi,au hata wakienda inafika hata mara moja kwa mwaka?
Mkuu inawezekana kuna vitu huvijui kabisa kuhusu haya magari,au unajua kiasi,au unajua ila upo katika macho yaliyofunikwa au umekariri tu.
Kwa mfano,ukimpatia afisa elimu TOYOTA KLUUGER ya 20M ni maeneo gani anaweza ashindwe kufika kabisa kisa hana usafiri?
Mchina ambaye ameweka madubu yake ameweka hadi vijiji vya ndani ndani huko kabisa na bado anayafuatilia zaidi ya mara moja kwa wiki na anatumia Kluger.
Mkuu,bado huamini kama hata manunuzi na matumizi ya hizo gari ni utumiaji mbovu wa pesa zetu?
LandCruiser sio chini ya 120M,mkuu,ukinunua Kluger moja na NISSAN X TRAIL MOJA ambazo hazizidi hata 40M ukampatia afisa elimu huyo huyo kwa matumizi ya miaka hiyo mitano hadi sita,je hayo magari hayatofika?
Hebu tuambiane UKWELI Kwanza mkuu
 
Gari ukiitumia vizuri mkuu inakaa hata miaka 20.
Kuna vijana mtaani wanajiita team cruiser,ipo moja waniita KING ABK (T....ABK),hiyo gari ina zaidi ya 20 yrs na bado iko vizuri mno mkuu
 
Kwani uifananishe tu TOYOTA IST na LandCruiser?
Kwanini huifananishi NISSAN X TRAIL,KLUGER, HARRIER OLD MODEL nk??
Hayo mazingira unayoyasema hapo ni mazingira gani?
Sehemu korofi zooote kuna muda wa kwenda sio wakati ambapo miundombinu haipitiki.
 
Huyu ni aidha hajui magari ama nae ni mnufaika...
 
Reactions: y-n
Gari ukiitumia vizuri mkuu inakaa hata miaka 20.
Kuna vijana mtaani wanajiita team cruiser,ipo moja waniita KING ABK (T....ABK),hiyo gari ina zaidi ya 20 yrs na bado iko vizuri mno mkuu
Hizo gari muda wake ni mkubwa, basi tu serikali ni wafujaji wa pesa.
 
Reactions: y-n
Tena haya ma DFPA madreva wanakula nayo Mbuzi sana, anyway magari mengi yaliyonunulia kwa hela ya uma watu wanahujumu sana.

Kuna jamaa niliwahi kufanya nae kazi mahara fulani, alikuwa akiiba Mafuta haswa, ilifikia hatua mpaka akawa anafungua hata baadhi ya spea na kuuza then anafunga vitu vyaajabu ajabu ili mradi gari linatembea.

Dreva wengi sijui ni Wachawi [emoji23][emoji23][emoji23], lkn nahisi management husika tu hawazingatii sana
 
Bila kuwa na kikosikazi cha siri cha kuyafuatilia yanavyotumika haitasaidia Mh. Waziri Mkuu, labda huko Dodoma na Dar, ila huku Idindilumunyo tunashuhudia mengi
 
Hoja yangu miaka mitano ni sawa tu kwa kuwa magari mengi ya serikali yanafanya kazi katika mazingira magumu, lakini pia huwa zinatumika ktk shughuri mbalimabali ambazo zinafanya haya magari kutumika sana
Unakuta gari la afisa elimu wa manispaa ya Morogoro kwa mfano linapelekwa kukimbiza mwenge Ifakara, Mahenge ni kweli lazima lichoke
 
Unakuta gari la afisa elimu wa manispaa ya Morogoro kwa mfano linapelekwa kukimbiza mwenge Ifakara, Mahenge ni kweli lazima lichoke
Hivyo likikimbiza mwenge linaharibika?
 
Hivyo likikimbiza mwenge linaharibika?
Uchakavu wa gari linalotumika manispaa ambako barabara zake nyingi ni lami na lile linalokwenda vijijini unatofautiana kwa kiasi kikubwa sana, maana yangu ni kwamba mtu wa manispaa anaweza kulaumiwa gari lake linachakaa kumbe wakati mwingine linaingizwa kwenye shughuli zisizo za manispaa
 
Afadhali maana jamaa wakija na mavi8 bar wanatuchukulia sana mamanzi wetu

Ova
 
Hivi dereva wa serikali lazima uwe na elimu ya kidato cha nne pekee? Vipi kama una ka diploma kako hakana mchongo humu kitaani ila una mavyeti yote ya udereva, hauwezi kutoboa?
 
Waziri Mkuu amefeli sana kwenye kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za nchi hii maskini yenye vijana wengi wasio na ajira .

Hivi kuna tatizo la wasomi au ajira !!
Nchi ajabu sana.
Mwaka jana tu kuna mkurugenzi alinunua gari ya mil. 400 kwa ajili ya kutembelea?


Ukifika kwenye Halmashauri zote kuna magari mengi sana yamehapakiwa kwa sabau ya pancha tu kwenye tairi halafu bado anaagiza magari mengine 184 + kwa kodi za maskini.
Kwa nini wasipige mnada yale yaliyopakiwa kuwa kwenye maofisi ha serikali ndipo wanunue mengine.
Kuna Ofisi moja gari limepakiwa kwa miaka saba sasa lakini linapigiwa gharama za mafuta kila mwezi. Wizi matimizi mabaya vimemshinda PM . Wakishindwa wajiuzulu tu sio kungangania wakati hawana jipya.
 
Ni Hilux Mkuu, Hata mimi nimeshangaa O km inapigiwa hesabu ya 5yrs
 
Reactions: y-n
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…