Waziri Mkuu Majaliwa: Corona imepungua Dar na Wagonjwa waliolazwa Wamepungua

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Akiongea baada ya swala ya Eid jijini Dodoma, Waziri Mkuu Mh. Majaliwa amesema idadi ya wagonjwa wa Corona imepungua sana nchini.

Amesema hadi leo asubuhi taarifa alizonazo hospitali nyingi hazina wagonjwa na chache zilizobaki wagonjwa wamepungua sana.

Kwa mfano Amana mgonjwa 1, Mloganzila 1, Agakhan 11, Kibaha 16 na Dodoma kuna wagonjwa 3.

Na wagonjwa wote wana hali nzuri wanasubiri kuruhusiwa kasoro Agakhan wagonjwa 4 bado wako katika uangalizi.

Pamoja na yote Mh. Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na kuvaa barakoa.

Source: Upendo Tv Habari
 
Wamepona mfano mzuri Piere wa Keko!
Na yule aliyepelekwa Kairuki jana ambaye PM na mtandao wake wote bado hajafahamu? Yani kukaa Dodoma basi ndo akae kiporipori asijue mambo ya mjini? Yule vipi? Naye amepona au?
 
U

Meambiwa hizo hospitali nyingine hazina wagonjwa..... Uwe unaelewa bwashee!
 
Sasa bwashee nitamuamini vipi kama tu jana Hassan Abbas kapeleka vyombo vyote vya habari chaka kwa ku post ndege hewa? Huyu naye muongo tu maana naongea nina uhakika na taatifa zangu bwashee. Huko kambini wamejaa waongo na wapotoshaji ndiyo maana siwasikilizi hata habari zao siwezi kunukuu bwashee.
 
Bwashee kwn hujakwenda ktk bonanza aliloandaa Bashite?Hyo korona mbna imekwisha zaman tu
Akiongea baada ya swala ya Eid jijini Dodoma waziri mkuu mh Majaliwa amesema idadi ya wagonjwa wa Corona imepungua sana nchini.

Amesema hadi leo asubuhi taarifa alizonazo hospitali nyingi hazina wagonjwa na chache zilizobaki wagonjwa wamepungua sana

Kwa mfano Amana mgonjwa 1, Mloganzila 1, Agakhan 11, Kibaha 13 na Dodoma kuna wagonjwa 3.
Na wagonjwa wote wana hali nzuri wanasubiri kuruhusiwa kasoro Agakhan wagonjwa 4 bado wako katika uangalizi.

Pamoja na yote mh Majaliwa amewataka watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na kuvaa barakoa.

Source Upendo tv habari!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nisaidieni kumshukuru Mungu. Mjomba wangu Deo, alipata Covid akapambana akapona, bahati mbaya sana mke wake aliyekuwa na ujauzito wa wiki 36 alipata maambukizi. Tarehe 1 mwezi huu alizidiwa na mjomba alizunguka naye kwa masaa 12 akikataliwa kupokelewa kwenye hospitali 6 Dsm. Deo ni mfanyabiasha mdogo sana lakini ameishika sana imani yake. Dakika za mwisho aliamua kwenda Agakhan kujaribu tu, maana pale hupokelewa watu maalum.

Kwa muujiza alipokelewa mkewe akiwa na hali mbaya sana. Kesho yake alifanyiwa operation mtoto akatolewa akiwa mzima. Mama alizidiwa na akakaa ICU kwenye ventilator kwa wiki mbili. Hatimae leo ameruhusiwa kutoka hospitali. Deo ni mtu wa kujitoa sana kwa watu. Bill ilikaribia 40m imechangwa na jamaa na marafiki kupitia group la whatsup alililianzisha.
*Utukufu, Heshima, Mamlaka na Adhama zina wewe MUNGU*
 
Duh! Huo kweli ulikuwa mtihani.
 
Back
Top Bottom