Waziri Mkuu Majaliwa: Corona imepungua Dar na Wagonjwa waliolazwa Wamepungua

Waziri Mkuu Majaliwa: Corona imepungua Dar na Wagonjwa waliolazwa Wamepungua

Hivi ni kweli inamaanisha Corona imepungua kiasi hicho au ni watu wameamua kutokwenda hospitali baada ya habari za kunyanyapaa wagonjwa na kutelekezwa, pamoja na yale yaliyotokea amana?. Au ni vyote kwa pamoja?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akiongea baada ya swala ya Eid jijini Dodoma, Waziri Mkuu Mh. Majaliwa amesema idadi ya wagonjwa wa Corona imepungua sana nchini.

Amesema hadi leo asubuhi taarifa alizonazo hospitali nyingi hazina wagonjwa na chache zilizobaki wagonjwa wamepungua sana.

Kwa mfano Amana mgonjwa 1, Mloganzila 1, Agakhan 11, Kibaha 16 na Dodoma kuna wagonjwa 3.

Na wagonjwa wote wana hali nzuri wanasubiri kuruhusiwa kasoro Agakhan wagonjwa 4 bado wako katika uangalizi.

Pamoja na yote Mh. Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na kuvaa barakoa.

Source: Upendo Tv Habari

Ingekuwa vizuri kama angetuambia/angetupa takwimu za wagonjwa walikuwa wangapi, wamepona wangapi na wamefariki wangapi.

Pia angetuambia kama kweli kwa kipindi hiki wagnjwa wa corona wanaende hospitali au wanajiugulizia nyumbani.

Anaweza kutoa hizo takwimu alizo toa laikini ni vizuri kujua kuwa wagonjwa wengi wanaogopa kwenda hospitali kutokana na huduma wanazo pewa kutokuwa rafiki, hivyo wanaaomua kujitibu wenyewe nyumbani
 
Mh. Rais kwa maono na ujasiri wake awe wa kwanza kuitangazia Tanzania na dunia ukweli,hakuna tiba wala hatuna uwezo kukabiliana na corona bali kwa uwezo wa Mungu na kinga ya mwili. Hivyo maisha yaendelee kama kawaida. Tahadhari iwe kwa wenye upungufu wa kinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani wagonjwa wamebaki mikoa ya Daslamu, pwani na dodoma tu?
Mikoa mingine haina wagonjwa wa Corona?
Halafu kwanin wasiseme kua daslamu ina wagojnwa kadhaa, dodo.a ina wagonjwa kadhaa kuliko huu utaratibu wa kutaja hospitali afu mikoa mitatu tu.
 
Kataa wagonjwa mahospitalini kisha tangaza ugonjwa haupo. Huu ni ukatili wa hali ya juu sana.

Halafu hawataji Zanzibar as if Zanzibar siyo Tanganyika. The issue hapa ni simple huenda Zanzibar walikuwa wanaogopa kudanganya kwa sababu wanaogopa kuharibu swaumu zao. Wale wana uislamu fulani hivi unaowatia hofu
 
Wamepona mfano mzuri Piere wa Keko!

PM anachekesha walionuna. Wananchi wanajua kila kinachoendelea ila wako kimya kwa kuhofia kundi la watu wasiojulikana. Kwa maneno marahisi wananchi wameamua kujiongeza kwenye hili gonjwa. Kizazi za kulishwa data fake kiliisha kabla ya ujio wa smartphone.
 
Nisaidieni kumshukuru Mungu. Mjomba wangu Deo, alipata Covid akapambana akapona, bahati mbaya sana mke wake aliyekuwa na ujauzito wa wiki 36 alipata maambukizi. Tarehe 1 mwezi huu alizidiwa na mjomba alizunguka naye kwa masaa 12 akikataliwa kupokelewa kwenye hospitali 6 Dsm. Deo ni mfanyabiasha mdogo sana lakini ameishika sana imani yake. Dakika za mwisho aliamua kwenda Agakhan kujaribu tu, maana pale hupokelewa watu maalum.

Kwa muujiza alipokelewa mkewe akiwa na hali mbaya sana. Kesho yake alifanyiwa operation mtoto akatolewa akiwa mzima. Mama alizidiwa na akakaa ICU kwenye ventilator kwa wiki mbili. Hatimae leo ameruhusiwa kutoka hospitali. Deo ni mtu wa kujitoa sana kwa watu. Bill ilikaribia 40m imechangwa na jamaa na marafiki kupitia group la whatsup alililianzisha.
*Utukufu, Heshima, Mamlaka na Adhama zina wewe MUNGU*
Mungu ashukuriwe! kumbe wangonjwa waweza kuwa hawaonekani mahospitalini kumbe ni kwasababu hawapokelewi

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Na yule aliyepelekwa Kairuki jana ambaye PM na mtandao wake wote bado hajafahamu? Yani kukaa Dodoma basi ndo akae kiporipori asijue mambo ya mjini? Yule vipi? Naye amepona au?
Si mmoja..avai vilinda miiba miguuni.Kairuki na 4
 
Kwa hiyo muda si mrefu tunafunga hospitali zote zilizoteuliwa kwa ajili ya corona. Mungu anatupenda sana sana hata kipimo hakipo
 
Nisaidieni kumshukuru Mungu. Mjomba wangu Deo, alipata Covid akapambana akapona, bahati mbaya sana mke wake aliyekuwa na ujauzito wa wiki 36 alipata maambukizi. Tarehe 1 mwezi huu alizidiwa na mjomba alizunguka naye kwa masaa 12 akikataliwa kupokelewa kwenye hospitali 6 Dsm. Deo ni mfanyabiasha mdogo sana lakini ameishika sana imani yake. Dakika za mwisho aliamua kwenda Agakhan kujaribu tu, maana pale hupokelewa watu maalum.

Kwa muujiza alipokelewa mkewe akiwa na hali mbaya sana. Kesho yake alifanyiwa operation mtoto akatolewa akiwa mzima. Mama alizidiwa na akakaa ICU kwenye ventilator kwa wiki mbili. Hatimae leo ameruhusiwa kutoka hospitali. Deo ni mtu wa kujitoa sana kwa watu. Bill ilikaribia 40m imechangwa na jamaa na marafiki kupitia group la whatsup alililianzisha.
*Utukufu, Heshima, Mamlaka na Adhama zina wewe MUNGU*
Mkuu hii kama kweli basi kuna watu watapata laana kubwa sana.
Unawezaje kukataa kumtibia mama mjazito aliye zidiwa?

Unataka kupoteza maisha ya watu wawili kwa mpigo mmoja!!
Kama uongo basi na laana itawaendea wenye kutunga habari za kuogofya kama hizi, maana wanatia watu hofu kubwa mno. Hii hofu inaweza kumuuwa mtu akipata huu ugonjwa.

BTW, Deo na mkewe walijuaje kama wanachoumwa ni COVID-19?
Walipimwa na kupewa maibu kisha wakakataliwa kuhudumiwa hospital hadi watakapo pona?
 
Back
Top Bottom