Nisaidieni kumshukuru Mungu. Mjomba wangu Deo, alipata Covid akapambana akapona, bahati mbaya sana mke wake aliyekuwa na ujauzito wa wiki 36 alipata maambukizi. Tarehe 1 mwezi huu alizidiwa na mjomba alizunguka naye kwa masaa 12 akikataliwa kupokelewa kwenye hospitali 6 Dsm. Deo ni mfanyabiasha mdogo sana lakini ameishika sana imani yake. Dakika za mwisho aliamua kwenda Agakhan kujaribu tu, maana pale hupokelewa watu maalum.
Kwa muujiza alipokelewa mkewe akiwa na hali mbaya sana. Kesho yake alifanyiwa operation mtoto akatolewa akiwa mzima. Mama alizidiwa na akakaa ICU kwenye ventilator kwa wiki mbili. Hatimae leo ameruhusiwa kutoka hospitali. Deo ni mtu wa kujitoa sana kwa watu. Bill ilikaribia 40m imechangwa na jamaa na marafiki kupitia group la whatsup alililianzisha.
*Utukufu, Heshima, Mamlaka na Adhama zina wewe MUNGU*