Waziri Mkuu Majaliwa, kweli tangu awamu ya tano iingie madarakani gharama za maisha hazijapanda? Kuwa na huruma kwa Watumishi wa Umma

Waziri Mkuu Majaliwa, kweli tangu awamu ya tano iingie madarakani gharama za maisha hazijapanda? Kuwa na huruma kwa Watumishi wa Umma

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Ndugu zangu wana JF, majibu ya PM Kassim Majaliwa yanashangaza sana na kutia ukakasi. Majibu aliyotoa kwa mbunge wa Konde kuwa kuongeza mishahara huongez gharama za maisha ni fedheha kubwa kwa watumishi wa umma.

Hivi PM Majaliwa tokea umekuwa waziri mkuu wa Tanzania unataka kusema kuwa gharama za maisha hazijabadilika? Kwamba bei ya sukari ni ileile tangu mwaka 2015?

Vipi kuhusu gharama za matibabu nazo ni zilezile tangu mwaka 2015?

Gharama za kupanga majumba nazo zimepungua kisa tu serikali haijaongeza mshahara?

Mbona mkuu wa kaya alishanukuliwa akisema haongezi mishahara watumishi wa umma sababu anataka akamilishe mambo muhimu kwa taifa? Na akikamilisha ataongeza nyongeza kubwa. Hii ya kudai kuwa serikali inakwepa kusababisha gharama za maisha kuwa juu inatoka wapi?

Ukweli ni kuwa watumishi wa umma hawajapata nyongeza ya mishahara kwa miaka mitano,lakini gharama za maisha zimepanda. Majibu yako PM Majaliwa hayafai na sio mazuri kwa watumishi wa umma.
 
Huwa wakaongeza mshahara kimya kimya, wakitangaza watumishi huwa wanapandiahiwa Bei ya bidhaa.
 
Majaliwa Kasimu nae amekuwa mchumia tumbo tu. Yale majibu hata ccm wenyewe mule mjengoni walimdharau
 
Halafu serikali inatapeli wananchi kuwa knna meli zinashusha mafuta bandarini. Kweli kuingia madarakani kwa wizi wa kura ni janga kwa nchi.
Mkuu masuala ya wizi wa kura yanatoka wapi?
 
Back
Top Bottom