Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, madarakani ameweza kutekeleza miradi yote ya kimkakati iliyoasisiwa na watangulizi wake akiwemo Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri Mkuu amesema Rais Samia ametimiza ahadi aliyoitoa kwa Watanzania, mara alipoingia madarakani ya kuwa hakuna mradi utakaosimama chini ya uongozi wake, na kwamba ataendeleza kila kilichoanzishwa na watangulizi wake.
Majaliwa pia amesema Rais Dkt. Samia amefanikiwa kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi mikubwa ya Maendeleo, pamoja na ya huduma za jamii inayowagusa wananchi wote hadi vijijini, kwenye sekta za afya, elimu na maji.