Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Utajua menywe bana...hawapendagi kupewa feedback, wao mapambio ...na dhambi za kutekaKwahiyo Kiongozi wetu haaminiki
Pwagu na pwaguzi siku hizi wapogo?Hivyo unamaanusha majaliwa hajaanza leo uongo
Hii ni habari njema sana.
Shida ni kwamba mtoa hii habari ana Historia ya kudanganya,, hii habari huenda pia ni muendelezo Wa ile tabia yake ya kusema uongo.
Nani wa kuzisimamia kama si BOT?! Kwa sasa riba za bank kuu ni 7% lakini mikopo ya bank mpaka 21% hivyo tatizo sio riba ya serikali au bank kuu bali tatizo ni banks zenyewe
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga Tsh. Trilioni moja kwa ajili ya mikopo kwa mabenki na taasisi za fedha kwa riba ya asilimia tatu ili mabenki na taasisi hizo zitoe mikopo kwa riba isiyozidi asilimia 10.
“Serikali imeendelea kulegeza masharti ya uanzishwaji wa ofisi za wakala wa mabenki, kushusha riba inayolipwa kwa akaunti za fedha za mitandao pamoja na kutenga shilingi trilioni moja kwa ajili ya mikopo kwa mabenki na taasisi za fedha kwa riba ya asilimia tatu ili mabenki na taasisi hizo zitoe mikopo kwa riba isiyozidi asilimia 10"
Ametoa kauli hiyo jana wakati akiahirisha Mkutano wa Tano wa Bunge Dodoma, Bunge limeahirishwa hadi Februari mosi, mwakani, Majaliwa amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2022/2023.
Akizungumzia kuhusu, riba kubwa za mikopo kutoka kwenye mabenki na taasisi za fedha, Waziri Mkuu amesema Serikali imekuwa ikichukua hatua madhubuti kupitia Benki Kuu ya Tanzania ikiwemo kupunguza kiwango cha akiba kinachowekwa na mabenki katika Benki Kuu.
Inatakiwa tujue Majaliwa anatumia id gani humu ili tuwe tunamuita anajisomea vitu kama hivi.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, amewataka watanzania wawapuuze Wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais Magufuli "Rais ana shughuli nyingi, Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini?" Leo asubuhi wakati nakuja huku nimeongea naye kwa simu na...www.jamiiforums.com