Waziri Mkuu Majaliwa: TANESCO imezalisha umeme zaidi ya mahitaji

Tuombe mvua zisikate tufaidi umeme, maana umeme wetu kwa kiasi kikubwa unategemea maji.
Vinginevyo huu ndiyo muda ambao serikali inatakiwa kuongeza mashine pale Kinyerezi ili ikiisha El Nino tujipange na La Nina kwa mitambo ya gesi.
 
Ni lini waliwacha kusambaza umeme?
 
Wakarabati na miundo mbinu yake ...manake kuna maeneo bado umeme unakatika ovyo na kurudi
 
Nani wa kuwaamini hawa watu?
Haponulipo kuna umeme au hakuna?

Amini macho yako.


Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Mimi nawasifu TANESCO kipindi hiki cha mvua kali za nasika zilizochanganyika na elnino zimekutana lakini umeme unapatikana bila hitilafu kubwa, ni hatuwa kubwa sana ya maboresho na mabadiliko (reforms) kiutendaji waliyopiga.

naamini miundombinu aliyokuwa anashughulikia januari Makamba inazaa matunda yake kipindi hiki.
 
Ndiyo akili za watanzania, wanampongeza mnyama aliyenaswa badala kumpongeza aliyetega mtego,
 
Ni jambo jema kwamba kuna uzalishaji wa kutosha. Hata hivyo Tanesco wajipange kuongeza uzalishaji. Ni hakika itafika wakati, kama uzalishaji hauongezeki, mahitaji ya umeme yatazidi uzalishaji.
 
Haa Ila Mkuu
Sasa Mimi Niseme Nini Wakati Sukari Haipatikani
HIi miezi miwili niliyokuwepo nchini nimetembelea familia zaidi ya 1000 wote wanakunywa chai sasa sijui wewe unaishi wapi kusiko patikana sukari!
 
Rais Magufuli ni mzima anaendelea kuchapa kazi.
 
HIi miezi miwili niliyokuwepo nchini nimetembelea familia zaidi ya 1000 wote wanakunywa chai sasa sijui wewe unaishi wapi kusiko patikana sukari!
Haa Haa Mkuu Umetoa Majibu Vile Vile Wanavyotoaga Wenyewe
Kwahiyo Sukari, Mafuta Yapo Na Yanauzwa Hadharani
ila Kama Moto Upo Mbinguni Sijui..........Utaepukaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…