mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,126
- 5,068
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Tanzania itandelea kuwa mstari wa mbele kuisaidia Msumbiji katika kukabiliana na vitendo ya kigaidi.
Aliyasema hayo jana alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa kujadili usalama katika eneo la Kusini Mashariki mwa Afrika, hususan nchini Msumbiji na maeneo ya Jirani (Aqaba Process).
Mkutano huo ulifanyika katika mji wa Aqaba, nchini Jordan.
“Tanzania tutaendelea na ushiriki wetu wa kuisaidia Msumbiji kwa kiwango wanachohitaji. Lengo ni kuhakikisha tunauondoa kabisa ugaidi nchini humo, tunapunguza hatari ya magaidi kuingia nchini Tanzania, pamoja na kuwasaidia kwa hali na mali wananchi wake kuendelea na shughuli zao,” alisema.
Alisema kuwa mkutano huo pia umepokea mapendekezo mbalimbali kutoka kwa Msumbiji na wadau wa Aqaba Process kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano na kuisaidia Msumbiji kukabiliana na changamoto za ugaidi.
“Eneo linaloshambuliwa ni kaskazini mwa Msumbiji ambalo ni kusini mwa nchi yetu, hivyo ushiriki wetu umekuwa ni muhimu sana,” alisema.
Mkutano huo ambao umeitishwa na Mfalme Abdullah II wa Jordan ni wa tatu tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015 na huwakutanisha viongozi wakuu wa nchi za ukanda wa Mashariki mwa Afrika, lengo likiwa ni kujadili changamoto za ugaidi na namna ya kuudhibiti.
Baadhi ya viongozi walioshiriki katika mkutano huo ni Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi, Rais wa Rwanda, Paul Kagame na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi
Chanzo: Habari Leo