Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema ni muhimu kwa Tanzania kuzingatia Sera za nje na kuimarisha mahusiano mazuri na mataifa mengine huku ikijikita zaidi katika kujitegemea kiuchumi.
Majaliwa ametoa kauli hiyo Bungeni Jijini Dodoma leo February 06,2025 wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, George Mwenisongole ambaye alitaka kufahamu kuhusu mipango ya Serikali kulingana na mabadiliko ya sera za nje ya nchi ambazo zinatajwa kuathiri sera za elimu, afya na uchumi za Tanzania.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa licha ya mafanikio haya ya kidiplomasia, nchi inapaswa kujiimarisha kiuchumi ili kupunguza utegemezi.
"Ni muhimu kuzingatia Sera za nje. Rais Samia ameendelea kuifanya nchi hii kuwa na mahusiano na mataifa mengi duniani. Marekani ni moja kati ya nchi hizo. Muhimu kwetu, pamoja na upana huu wa mahusiano, ni kuhakikisha tunajiimarisha na kuwa na uwezo wa ndani wa kutekeleza mipango yetu. Bajeti zetu zinapaswa kumudu sekta zote muhimu kama afya, elimu, na maji, pamoja na maeneo mengine tuliyokubaliana na mataifa husika," alisema Majaliwa.
Aliongeza kuwa Tanzania ina uwezo wa kujitegemea kutokana na maliasili na rasilimali ilizonazo, na akatoa wito kwa Watanzania kushirikiana katika kuzitumia kwa maendeleo ya taifa.
"Kazi iliyopo sasa ni kuhakikisha tunashirikiana na kutumia rasilimali tulizonazo kujenga uchumi wa ndani," alihitimisha Waziri Mkuu.
Soma, Pia:

Kila anapohutubia au kuongea lazima amtaje Daktari Samia Suluhu Hassan. 🤔 Ni kweli kwamba yeye hana maono au mawazo yake binafsi au yeye ni mwangwi wa SSH⁉️