Waziri Mkuu Majaliwa: Tanzania lazima ijiimarishe Kiuchumi ili kuepuka utegemezi kutoka mataifa mengine duniani

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema ni muhimu kwa Tanzania kuzingatia Sera za nje na kuimarisha mahusiano mazuri na mataifa mengine huku ikijikita zaidi katika kujitegemea kiuchumi.

Akizungumza Bungeni leo, Majaliwa alieleza kuwa juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan zimeifanya Tanzania kuwa na mahusiano mapana na mataifa mengi duniani, ikiwemo Marekani na nchi nyingine. Hata hivyo, amesisitiza kuwa licha ya mafanikio haya ya kidiplomasia, nchi inapaswa kujiimarisha kiuchumi ili kupunguza utegemezi.

"Ni muhimu kuzingatia Sera za nje. Rais Samia ameendelea kuifanya nchi hii kuwa na mahusiano na mataifa mengi duniani. Marekani ni moja kati ya nchi hizo. Muhimu kwetu, pamoja na upana huu wa mahusiano, ni kuhakikisha tunajiimarisha na kuwa na uwezo wa ndani wa kutekeleza mipango yetu. Bajeti zetu zinapaswa kumudu sekta zote muhimu kama afya, elimu, na maji, pamoja na maeneo mengine tuliyokubaliana na mataifa husika," alisema Majaliwa.

Aliongeza kuwa Tanzania ina uwezo wa kujitegemea kutokana na maliasili na rasilimali ilizonazo, na akatoa wito kwa Watanzania kushirikiana katika kuzitumia kwa maendeleo ya taifa.

"Kazi iliyopo sasa ni kuhakikisha tunashirikiana na kutumia rasilimali tulizonazo kujenga uchumi wa ndani," alihitimisha Waziri Mkuu.

Hillo Ndiyo wazo zuri lakini lisiishie mdomoni lazima kuwe na mipango mikakati, (strategy formulation to reach smart goals)
 
Anazungumzia Tanzania kujitegemea kiuchumi na wakati huo serikali yake inayotegema mikopo na misaada inafanya matumizi ya anasa kwenye mambo ambayo hayana umuhimu na pesa nyingi zinaishia kwenye kuhonga na kununua wapinzani, hiyo ni ndoto ambayo haiwezi kutimia chini ya ccm haina watu wanao itakia mema nchi zaidi ya matumbo yao
 
Asanti kwa maoni yako.🙏

unaonaje hili suala la kujitegemea kiuchumi? kumbuka SaDC in soko kubwa sana lina watu takriban 300milion + na per capita last time I checked approx $2000 unafikiri tutaweza kama nchi kuepuka utegemezi, na kuvushwa kwenda mu nchi tunayoitaka?
Issue hapa ni mindset zetu za kijinga tu kuamini kila kitu ni Ulaya na Marekani, soko tunalo sababu SADC ina watu zaidi ya milioni 500 ambapo ni soko kubwa sn tungeamua tu alzeti, sukari, ngano, mazoo ya mifugo, mbaazi, kahawa na pamba kuuziana ndani ya SADC tungepiga pesa na kuondokana na utengemezi, pia lazima tuwekeze kwenye technolojia tuwe na viwanda vya magari yetu wenyewe na vito vya thamani
 
Nashukuru, maoni yangu ni haya, 1. Tuache betting watu wafanye kazi 2. Matumizi makubwa na ya anasa serikalini yadhibitiwe hakuna cha misafara 3. Ajira zisiwe za upendeleo nafasi zote zitangazwe watu waombe washindanishwe tupate watu wazuri kuanzia Waziri mpka mfagiaji. 4. Pombe kali ziondolewe na hakuna kuingia bar kabla ya saa 12 jioni na mwisho saa 5 kamili usiku. 5. Wabunge wasilipwe sitting allowance na mishahara yao ishushwe isizidi 2M ili waingie watu wazuri na siyo hawa wasaka utajiri, viti maalum vifutwe bungeni. 6. Ajira zote ziwe za mikataba mwisho miaka 10. 7. Wezi na mafisadi wafiliwe na kufungwa na kusiwe na kinga kwa viongozi. 8. Elimu yetu iwe ni ya vitendo kwa 90% na siyo kukaa darasani. 9. Wataalam walipwe vizuri kuliko wanasiasa. 10. Viongozi wakutumia magari ya umma wawe ni Rais, Makamu, Spika, PM na Jaji Mkuu pekee na vyeo vya RC/DC/DAS vifutwe kabisa. Asante
Asante
 
Hizi ulizo orodhesha ndizo sera KUNTU , ila sasa . . . . mmh hiiiiii. .. . !
 
Tutajitegemea na kuimarisha uchumi kivipi kama viongozi wanatumia hela za kodi kama maji?!
Anasa, masherehe, masafari, misururu ya magari makubwa, maposho kebekebe, kulipa wasanii bila uchungu nk nk.
Hatuko serious kabisa!
 
Shuka sasa tulikumbuke kumekucha, tuepuke mnada !
nimeona hii hapa jukwaani👉
Tutajitegemea na kuimarisha uchumi kivipi kama viongozi wanatumia hela za kodi kama maji?!
Anasa, masherehe, masafari, misururu ya magari makubwa, maposho kebekebe, kulipa wasanii bila uchungu nk nk.
Hatuko serious kabisa!
CHADEMA tupo serious mkulu.

nyie ccm kama hamko serious mtupishe.

hatahivyo mkulu usikate tamaa
 
Dr Samia S. Hassan alikuwa ni VP wakati wa JPM

Dr. Philipo I. Mpango alikuwa ni Waziri wa Fedha wakati wa JPM

Mwl. Majaliwa K. Majaliwa alikuwa ni PM wakati wa JPM

Dr JPM alikuwa Rais wakati huo ambapo sera na maono yake ilikuwa Nchi kuanza kujitegemea na kupunguza kuomba omba misaada na madeni

Kimewashinda nini Viongozi hao niliowataja kuenzi na kufata Sera za JPM, hadi kuanza kushtuka sasa baada ya USA Chini ya Trump kuminya misaada?

Watu wangu wanaangamia Kwa kukosa maarifa 🙌
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema ni muhimu kwa Tanzania kuzingatia Sera za nje na kuimarisha mahusiano mazuri na mataifa mengine huku ikijikita zaidi katika kujitegemea kiuchumi.

Akizungumza Bungeni leo, Majaliwa alieleza kuwa juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan zimeifanya Tanzania kuwa na mahusiano mapana na mataifa mengi duniani, ikiwemo Marekani na nchi nyingine. Hata hivyo, amesisitiza kuwa licha ya mafanikio haya ya kidiplomasia, nchi inapaswa kujiimarisha kiuchumi ili kupunguza utegemezi.

"Ni muhimu kuzingatia Sera za nje. Rais Samia ameendelea kuifanya nchi hii kuwa na mahusiano na mataifa mengi duniani. Marekani ni moja kati ya nchi hizo. Muhimu kwetu, pamoja na upana huu wa mahusiano, ni kuhakikisha tunajiimarisha na kuwa na uwezo wa ndani wa kutekeleza mipango yetu. Bajeti zetu zinapaswa kumudu sekta zote muhimu kama afya, elimu, na maji, pamoja na maeneo mengine tuliyokubaliana na mataifa husika," alisema Majaliwa.

Aliongeza kuwa Tanzania ina uwezo wa kujitegemea kutokana na maliasili na rasilimali ilizonazo, na akatoa wito kwa Watanzania kushirikiana katika kuzitumia kwa maendeleo ya taifa.

"Kazi iliyopo sasa ni kuhakikisha tunashirikiana na kutumia rasilimali tulizonazo kujenga uchumi wa ndani," alihitimisha Waziri Mkuu.

Huyu ndiye aliyesema Magu yupo ofisini ana chapa kazi kumbe kafa😡
 
Nashukuru, maoni yangu ni haya, 1. Tuache betting watu wafanye kazi 2. Matumizi makubwa na ya anasa serikalini yadhibitiwe hakuna cha misafara 3. Ajira zisiwe za upendeleo nafasi zote zitangazwe watu waombe washindanishwe tupate watu wazuri kuanzia Waziri mpka mfagiaji. 4. Pombe kali ziondolewe na hakuna kuingia bar kabla ya saa 12 jioni na mwisho saa 5 kamili usiku. 5. Wabunge wasilipwe sitting allowance na mishahara yao ishushwe isizidi 2M ili waingie watu wazuri na siyo hawa wasaka utajiri, viti maalum vifutwe bungeni. 6. Ajira zote ziwe za mikataba mwisho miaka 10. 7. Wezi na mafisadi wafiliwe na kufungwa na kusiwe na kinga kwa viongozi. 8. Elimu yetu iwe ni ya vitendo kwa 90% na siyo kukaa darasani. 9. Wataalam walipwe vizuri kuliko wanasiasa. 10. Viongozi wakutumia magari ya umma wawe ni Rais, Makamu, Spika, PM na Jaji Mkuu pekee na vyeo vya RC/DC/DAS vifutwe kabisa. Asante
Ushauri mzuri
 
Waziri mkuu Mh Majaliwa amesema Sera ya Mambo ya nje ya Marekani Kwa Sasa ni kutotoa Msaada nchi za nje hivyo ni lazima Tanzania tujikite Kwenye kujitegemea

Mh Majaliwa amesema Msimamo wa Trump una athari kwa baadhi ya sekta Nchini hivyo msisitizo ni wananchi kuanza kujitegemea na si vinginevyo

PM Majaliwa ameongea haya bungeni Dodoma

Source Mwananchi

Kwako Lucas Mwashambwa
 
Anachofanya Trump ni kwamba, huwezi kwenda kinyume na maslahi ya wamarekani halafu bado wakaendelea kukupa pesa.

Marekani wataendelea kusaidia nchi ambazo zipo upande wao kama Kenya, Rwanda ila zile nchi zenye viburi na ambazo zimeonesha kuwa Pro-Russia kama Tanzania wata deal nao papendicularly.

We hushangai South Africa kukatiwa misaada na Marekani? Trend tunakoelekea huko, USAID itafumuliwa ila utakuja mfumo mwengine wa misaada ambao misaada itakuwa channelled kwa nchi rafiki wa Marekani tu
 
Waziri mkuu Mh Majaliwa amesema Sera ya Mambo ya nje ya Marekani Kwa Sasa ni kutotoa Msaada nchi za nje hivyo ni lazima Tanzania tujikite Kwenye kujitegemea

Mh Majaliwa amesema Msimamo wa Trump una athari kwa baadhi ya sekta Nchini hivyo msisitizo ni wananchi kuanza kujitegemea na si vinginevyo

PM Majaliwa ameongea haya bungeni Dodoma

Source Mwananchi

Kwako Lucas Mwashambwa
Msisitizo ni kwa serikali kuachana na matumizi ya anasa
 
Back
Top Bottom