Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa waumini wa dini mbalimbali nchini kuzingatia Sheria ya uhuru wa kuabudu wanapotekeleza ibada zao, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili kuhakikisha ibada hazivunji amani wala sheria za nchi.
"Tunapokuja kuabudu hapa, tuzingatie sheria ya uhuru wa kuabudu... Ilimradi hakuna uvunjifu wa amani na sheria za nchi. Huku kuabudu si tu watu wanakutana na kufanya wanavyotaka; pamoja na uhuru wa kuabudu, ipo sheria iliyoruhusu msikiti huu kuwa hapa, kanisa lile kuwa pale, na ndiyo iliyoruhusu wale wajenge na wakutane pale..." amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo leo, Juni 7, 2025, wakati wa Baraza la Eid al-Adh-ha, mara baada ya kuswaliwa kwa swala ya Eid kitaifa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.