Waziri Mkuu: Miradi yote ya awamu iliyopita itatekelezwa

Waziri Mkuu: Miradi yote ya awamu iliyopita itatekelezwa

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Baada ya hoja kadhaa wiki hii kuibuka za kumuacha Rais Samia Suluhu aidha Kuandika kitabu chake au aendelee na kilichopo, waziri mkuu wakati akihitimisha hoja yake ya bajeti, amesema serikali ya awamu ya sita itaendelea kukamilisha ahadi zikizotolewa wakati wa kampeni zilizopo kwenye ilani ya CCM ya mwaka 2020.

''Miradi yote ya kipaumbele iliyoanishwa kwenye ilani ambayo imeanza kutekelezwa na ile ambayo bado haijatekelezwa, yote itatekelezwa kuhakikisha tunafikia malengo ya chama cha mapinduzi kupitia serikali yake kwa kutekeleza na kusimamia miradi yote ya kimkakati'' Alisema waziri mkuu, Kassim Majaliwa.

Pia waziri mkuu amesema upo mpango wa tatu wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano umeweka kipaumbele cha kuendelea na miradi mikubwa ya kimkakati ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji hivyo jambo hilo halina matatizo.

 
Back
Top Bottom