Pre GE2025 Waziri mkuu: Mpango wetu CCM ni kuhakikisha wagombea wetu watakapopita kwenye maeneo yetu wasipate kazi kubwa kueleza miradi ya maendeleo

Pre GE2025 Waziri mkuu: Mpango wetu CCM ni kuhakikisha wagombea wetu watakapopita kwenye maeneo yetu wasipate kazi kubwa kueleza miradi ya maendeleo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akiwa ni mgeni rasmi kwenye mkutano Mkuu Maalum Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Itilima, mkoani Simiyu Februari 15, 2025 amesema mpango wa Chama hicho ni kuhakikisha kwamba wagombea wao hawapati shida kueleza miradi ya maendeleo kwenye eneo watakapopita.

"Mpango wetu Chama Cha Mapinduzi ni kuhakikisha kwamba wagombea wetu watakapopita kwenye maeneo yetu wasipate kazi kubwa kueleza miradi ya maendeleo kwenye eneo husika kazi hiyo itafanywa na wanaCCM mlipo kwenye eneo hilo"

Soma pia: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

 
Back
Top Bottom