Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akiwa ni mgeni rasmi kwenye mkutano Mkuu Maalum Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Itilima, mkoani Simiyu Februari 15, 2025 amesema mpango wa Chama hicho ni kuhakikisha kwamba wagombea wao hawapati shida kueleza miradi ya maendeleo kwenye eneo watakapopita.
"Mpango wetu Chama Cha Mapinduzi ni kuhakikisha kwamba wagombea wetu watakapopita kwenye maeneo yetu wasipate kazi kubwa kueleza miradi ya maendeleo kwenye eneo husika kazi hiyo itafanywa na wanaCCM mlipo kwenye eneo hilo"