Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho waliokabidhiwa jukumu la kusimamia mchakato wa kuchuja wagombea wa uchaguzi kutenda haki na kuepuka upendeleo.
Waziri Mkuu mstaafu Pinda ametoa kauli hiyo jijini Tanga mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la CCM la mkoa, ambalo kwa sasa linaendelea kukarabatiwa na limefikia asilimia 99 ya utekelezaji.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Amesema kiongozi bora hutambulika kwa tabia na matendo yake ndani ya jamii, hivyo ni muhimu kuhakikisha anachaguliwa mtu sahihi atakayeweza kuwaongoza Watanzania na kuwaletea maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.