Waziri Mkuu Mwingulu: Pamoja na Viongozi wa dini tutajenga taifa lenye haki

Waziri Mkuu Mwingulu: Pamoja na Viongozi wa dini tutajenga taifa lenye haki

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Januari 18, 2026, ameungana na waumini wa Kanisa Kuu la Anglikana la Roho Mtakatifu jijini Dodoma katika ibada ya Jumapili, ambapo amesisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kushirikiana na viongozi wa dini katika kulijenga Taifa lenye hofu ya Mungu, upendo, haki na uwajibikaji.

Akizungumza kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Dkt. Mwigulu amebainisha kuwa taasisi za dini zina nafasi ya kipekee katika kuhubiri maadili ya upendo, uvumilivu, na kuheshimiana, ambayo ndiyo nguzo kuu za amani na mshikamano wa kitaifa nchini Tanzania.

Katika hotuba yake iliyojikita katika misingi ya kiimani na kijamii, Waziri Mkuu amewakumbusha Watanzania kuwa amani inayoshuhudiwa nchini si jambo la bahati, bali ni matokeo ya jitihada za makusudi kati ya Serikali, familia, na taasisi za kidini.

Akitumia mstari wa Biblia kutoka kitabu cha Mika 6:8, amesisitiza kuwa unyenyekevu, kutenda haki, na kupenda rehema si maadili ya kidini pekee, bali ni misingi muhimu ya ustawi wa jamii na maendeleo endelevu ya Taifa. Ameongeza kuwa imani ya kweli inapaswa kutafsiriwa kwa vitendo vya uadilifu, bidii katika kazi, na kuheshimu sheria za nchi.

 
Back
Top Bottom