Waziri mkuu Pinda ametamka bungeni wanafunzi kutumia Tablet na PC

Waziri mkuu Pinda ametamka bungeni wanafunzi kutumia Tablet na PC

mkongongojo

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2014
Posts
245
Reaction score
156
Katika kipindi cha maswali na majibu bungeni kwa waziri mkuu aliwaeleza wabunge ya kwamba wanafunzi watatumia tablet pc mbadala wa kubeba vitabu.

Wakati wanafunzi wanakaa chini hakuna madawati, vyumba vya kusomea ni vibovu, mahabara na maktaba hakuna na umeme pia katika shule zetu.

Je hilo litafanyika kweli na uhalisia tuliyonayo au ni porojo tu?
 
Wanasiasa wapumbavu hawana haya kuudanganya umma.
-labda anachoongelea ni technology iliyopo na ambayo inaendelea kuwepo ila hio ipo na ni juhudi za myu binafsi kumiliki tablets na kuachana na madaftari ila sio juhudi ya serikali .
 
Katika kipindi cha maswali na majibu bungeni kwa waziri mkuu aliwaeleza wabunge ya kwamba wanafunzi watatumia tablet pc mbadala wa kubeba vitabu. Wakati wanafunzi wanakaa chini hakuna madawati, vyumba vya kusomea ni vibovu, mahabara na maktaba hakuna na umeme pia katika shule zetu. Je hilo litafanyika kweli na uhalisia tuliyonayo au ni porojo tu?

Waanze Bungeni kutumia hizo technologia kama sehemu ya mkakati wa kuhifadhi mazingira ili dunia iwe sehemu nzuri ya kuishi.

Embu oneni kwa kila chapisho ni lazima nakala zisizopungua 350 mpaka Bunge liishe hizo karatasi ni sawa na miti mingapi itakuwa imekatwa?
 
Hamna kitu hapo labda waseme ni ruksa kutumia lakini siyo kwamba wao ndiyo watazitoa kwa wanafunzi!!
 
Mi naona iwekwe sheria ya kuzuia watu wenye PhD na maprofesa kuwa wabunge na mawazir kwan hawa ni wanataaluma walobobea ktk tafiti leo anasimama anasema uongo hv wanaf wataelewa nin wanadhalilisha dictorate zai na pro zao
 
Back
Top Bottom