Waziri Mkuu: Tumesitisha Sunday school na Madrasa, tulichoruhusu ni Ibada tu tena zifanyike kwa muda mfupi kisha waumini waondoke

Waziri Mkuu: Tumesitisha Sunday school na Madrasa, tulichoruhusu ni Ibada tu tena zifanyike kwa muda mfupi kisha waumini waondoke

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri mkuu mh Kassim Majaliwa amesema kuna taarifa kuwa baada ya masomo kusitishwa kwa sababu ya Covid 19 watoto hao sasa wamekuwa wakienda makanisani na misikitini kwa ajili ya kujinza.

Mh Majaliwa amesisitiza kuwa alipokutana na maaskofu na mashehe walikubaliana kusitisha Huduma nyingine zote isipokuwa ibada tu.

Hivyo waziri mkuu amesema ni marufuku kwa watoto kukusanywa kwa kisingizio cha sunday school na madrasa na kwamba makanisa na misikiti itumike kwa shughuli za Ibada tu za kuliombea taifa tena kwa muda mfupi na baada ya Ibada waumini watawanyike mara moja.

Chanzo: Channel ten habari!
 
Viongozi wa makanisa na misikiti hamuoni aibu mkatangaza kusitisha ibada zenu?

Au ndio mnataka hadi serikali iwaambie fungeni nyumba zenu za ibada?

Kupitia kauli hii ya waziri mkuu nadhani kama watu wazima mnaojali afya za watanzania na nyie pia, mnapaswa kujiongeza.

Jiongezeni!
 
Kwahiyo wazazi waende wabebe ugonjwa wapeleke nyumbani kwa watoto na wafanyakazi waliobaki nyumbani? Kuombea taifa lipi sasa? Linaloenda kuambukizwa ibadani likaambukize nyumbani? Nini shida na hizi ibada? Tunataka kumfurahisha nani?
 
Elimu iongezwe bado watu hawajaelimika

FB_IMG_1586622743246.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa watu sijui vipi yaani!

Mikusanyiko huko misikitini na makanisani ni hatari hata kama watakaa kwa muda mfupi!
Huhitaji epidemiologist akwambie, Corona ni airborne disease kwa hiyo mikusanyiko tena ya watu wasio na masks ni hatari sana.
 
Angesitisha na ibada tu
Watu wasalie nyumbani

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app

hata mimi naishangaa serikali. Kufunga madrasa na sunday schools ni jambo zuri lakini nadhani kuachia ibada ziendelee tutakuwa tunarudisha nyuma mafanikio na faida za kufunga madrasa na sunday school.

Je, watoto hawaruhusiwi kwenye hizo ibada ambazo serikali imeruhusu ziendelee?

..
 
Muda mfupi ndo muda gani? Hahahaa Tanzania vituko haviishi.
 
Back
Top Bottom