Waziri Mkuu: Tumesitisha Sunday school na Madrasa, tulichoruhusu ni Ibada tu tena zifanyike kwa muda mfupi kisha waumini waondoke

Waziri Mkuu: Tumesitisha Sunday school na Madrasa, tulichoruhusu ni Ibada tu tena zifanyike kwa muda mfupi kisha waumini waondoke

JokaKuu,
Serikali inataka kujionyesha kwamba ina wacha Mungu, hivyo wanatoa nafasi ya upendeleo kwa nyumba za ibada, ni kama wanawatega viongozi wa dini ili huko mbeleni wawatumie kwa faida ya kisiasa.
 
Hali ni mbaya inafaa hata ibada zifanyike nyumbani kilamtu kivyake tusing'ang'anie kisa kunamtu alitoa kauli!!

Shida walimsifu amemshinda shetani sasa akistopisha ibada itakuwa kinyume kwamba shetani kamzidi... Kiukweli hiyo ni sababu ya kijinga, ibada zisimame tutasali kupitia mitandao na TV tuache ujuha maambukizi yanatisha!!

Joe Davie kule arusha anapambania kujaza waumini huko 'ETI' mji wa daudi huku akiwatoza mahela kwa nguvu zote. Huyu jamaa anatamaa ya Mali sana sasa hatutaki watu wafe hatakama ni wajinga!!
 
Ili kujikinga na hili janga usiwasikilize wanasiasa wala viongozi wa dini, sikiliza wataalamu wa afya.

Jana kwa bahati mbaya sana nilimsikia padri mmoja wa kikatoliki akihojiwa na VOA kuhusu kusitisha ibada akasema ibada ni mkusanyiko wa muhimu sana ndio maana hata serikali haijazuia.
 
"Ngoja tukusanyekusanye sadaka kwanza.... magari yetu yasikose mafuta...."

Mungu atusaidie kwa kweli maana tuna mzaha sana na huu ugonjwa kana kwamba sio tishio kwetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui hili suala lina manufaa kwa nani? ktk dini ya Uislaam ipo wazi tu kipindi kama hiki ibada inatakiwa kufanyika nyumban na hao viongozi wa din nadhani wanafikiria mno sadaka kuliko maslahi ya umma ni muda muafaka kusitishwa hii mikusanyiko tusisubir mpaka yatokee ni kutumia busara tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mheshimiwa Majaliwa funga tu milango ya nyumba za Mungu, au unangoja Watanzania wafe wote?

Mungu halazimiswi wala hapangiwi, muda wake ukifika Corona itaisha. Tahadhari ni muhimu zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
johnthebaptist, Kwamba ibada zikifanyika kwa muda mfupi ndio CORONA haiwezi kusambaa makanisani na msikitini
Siamini kama Waziri Mkuu mwenye akili timamu anaweza kuropoka hovyo namna hii. Angesema Bashite sawa tu lakini Majaliwa! Jamani Watanzania, tulimkosea nini Mungu hadi shetani anatupiga hivi?
 
Tafadhali soma tena ujumbe wangu kwa makini kisha upeleke ujinga wako huko nyumbani kwenu ukautulize huko kimya.
Duh kama maoni yangu yamekukera basi nisamehe sioni haja ya kuitana wajinga maana hapa hatulipwi wewe usiye mjinga na mie mjinga wote maoni yetu yanaishia humu humu JF tu.
 
Cjui hili suala lina manufaa kwa nan?ktk dini ya uislaam ipo wazi tu kipindi kama hiki ibada inatakiwa kufanyika nyumban na hao viongozi wa din nadhan wanafikiria mno sadaka kuliko maslahi ya umma ni muda muafaka kusitishwa hii mikusanyiko tusisubir mpaka yatokee ni kutumia busara tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Duu mkuu umegonga henyewe
 
Ili kujikinga na hili janga usiwasikilize wanasiasa wala viongozi wa dini, sikiliza wataalamu wa afya.

Jana kwa bahati mbaya sana nilimsikia padri mmoja wa kikatoliki akihojiwa na VOA kuhusu kusitisha ibada akasema ibada ni mkusanyiko wa muhimu sana ndio maana hata serikali haijazuia.
Kule Italy hawakujua umuhimu wa Ibada hadi Pope kahutubia kanisa bila waumini?
Huyo Padre ni wa kutilia shaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora angekaa kimya kuliko kulusha mawe juu ya mayai....nadhani viongozi, wa ccm wote nikama Mwigulu.
 
JokaKuu,
Serikali inataka kujionyesha kwamba ina wacha Mungu, hivyo wanatoa nafasi ya upendeleo kwa nyumba za ibada, ni kama wanawatega viongozi wa dini ili huko mbeleni wawatumie kwa faida ya kisiasa.
I totally agree with you.

Hapa nadhani Viongozi wa dini wachukue hatua wao wenyewe wasisubiri kuamriwa na serikali.
 
Back
Top Bottom