Waziri Mkuu: Tumesitisha Sunday school na Madrasa, tulichoruhusu ni Ibada tu tena zifanyike kwa muda mfupi kisha waumini waondoke

Uzuri ni kuwa wabongo watajipiga lockdown wenyewe. Kama wiki hii watakaokuwa kwenye ibada labda wafuasi wa gwajiboy.
Tena Dar ndio kabisa watu wanaweza kupotea makanisani, na ili kukwepa aibu,watatangaza kusitisha ibada kabla ya kukumbwa na aibu ya kukutana na mabenchi badala ya waumini.
 
UNAWASITISHA WATOTO BABA ZAO SI WATAULETA TU KAMA IBADA ZINAENDELEA DAH
MOLA TUNUSURU
 
Nimejiuliza Sana hili ... Inachukua Danika ngapi kuambukizana

Mkuu, corona ni kirusi cha ajabu sana, kwa ambae hajaelezwa na mgonjwa utaona kawaida tu.
Sio lazima mtu akutemee kama wengine wanavyodai.

Kuna tawi moja la Benki nimeingia tarehe 6, kulikuwa na wateja wengine. Leo hii,mlango wa tawi huo umefungwa, baada ya kupatikana wahudumu humo wana virusi.

Sasa jiulize teller na mteja kuna umbali na kioo katikati,lakini baadhi ya wateja waliokuwa humo,tayari wanavyo. Wanasakwa wengine waliohudumiwa humo. Hivyo, pengine kwenye kushika pesa, na hewa.

Nadhani swala la dakika ngapi, ni majaliwa tu
 
Kumbe dawa ya corona ni kukusanyika kwa muda mfupi!

The impression I am getting is that the commission tasked with leading the fight against the COVID-19 pandemic is not well versed with what challenges we are facing as a country!!
 
Mm nashangaa hawa mashekhe wanaacha mafunzo ya uislamu unaotutaka tufunge misikiti na tuswali majumbani ili kuepuka maambukizi na kuambukizi wenzetu huku tukiifuata kanuni za watawala na wataalamu wa afya
 
Haha nishasema Tanzania udini unawasumbua sana. Hawataki zuia watu kwenda makanisani wanaogopa kukosa kura mwaka huu? Acheni ushenzi kanisani si lazima mwende au misikitini mungu si vitabu vyenu vinasema yupo kila mahali?

Sasa kusanyikeni hata dakika tano muone, haha hana aibu kusema wakusanyike haraka wasepe? Kwani corona inahitajii saa nzima? Ni kitendo cha mtu moja kukohoa au kupiga chafya watu wote wa karibu wameudaka ndani ya sekunde moja tu. Upuuzi wa dini unawasumbua sana vichwa, mungu mungu haha maombi hayafiki tu?
 
makanisa ya kilokole mengi yameongeza siku za ibada badala ya kupunguza, watu wanasali jumatatu hadi jumapili alafu mafundisho yaleyale ya kutoa zaka malimbuko sadaka. Yaani shida tupu kichwa cha mwafrika, serikali isipojiangalia kwa jicho pana itazilaumu taasisi za dini lakini wananchi watailaumu serikali kwa uzembe huu....serikali kipindi hiki ilitakiwa isionee aibu mtu yeyote ama taasisi yeyote(usipoziba ufa utajenga ukuta), ukionea aibu mtu utaua watu wengi sana.

serikali iwe makini sana, ikiwezekana wasimamie taasisi za dini kama mtoto mdogo, kuna wanajeshi wanaoonekanaga msimu wa matukio maalum pekee...kwanini hao wasipewe kazi za kusimamia taasisi za dini kipindi hiki?, waingiao misikitini na makanisani wavae masks wakati wote ndio waingie ibada zao, wanawe maji, wakae mbalimbali kwenye viti,

muda wa ibada usizidi saa 1 na nusu yaani usizidi dakika 90, ibada iwe siku moja kwa wiki yaani ijumaa waswali waislamu, jumamosi wasabato na jumapili hao wengine wote waliosalia. Jamani serikali saidieni wananchi wenu ambao elimu zao ni duni, maisha yao ni duni, afya zao ni duni, kula yao ni duni (ishi yao duni). Mtahukumiwa mbinguni kwa mkitendacho duniani...tenda wema daima!!
 
NAKWEDE,
Wanazingua sana... Lakini, ni tatizo letu Waafrika - wagumu kuelewa.
Bahati mvaya haianzi nao. Hii ni kuhatarisha maisha. Inaa maana dunia nzima hawamjui Mungu? Kwenye hiyo idadi iliyotajwa,kumbukeni wamekutana na watu wangapi?

Ujue wapo waliosafiri. Wapo watakaokufa bila kutambua chanzo ni nini. Siasi haihusiani na corona wazee. Atakuja kulia kama mtoto,bahati mbaya wasioweza kupaza sauti ndo wahanga wakubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…