#COVID19 Waziri Mkuu: Tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake

#COVID19 Waziri Mkuu: Tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, Serikali haitamlazimisha mwananchi kuchanjwa chanjo ya corona. Amewataka Watanzania wapuuze upotoshaji unaosambazwa “Chanjo ni hiari tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake."

=========

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali haijamlazimisha na wala haitamlazimisha mwananchi kuchanjwa chanjo ya ugonjwa wa UVIKO 19, hivyo amewataka Watanzania wapuuze upotoshaji unaosambazwa kupitia mitandao ya kijamii.

“Hakuna aliyelazimishwa kuchanja chanjo hiyo na wala hakuna mahali palipoandikwa kwamba lazima wananchi wachanjwe. Chanjo ni hiari tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Julai 27, 2021) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Ruangwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nandagala ambapo amewasisitiza waendelee kuchukua tahadhari na kujikinga na UVIKO 19.

Majaliwa amesema Serikali imeleta chanjo hiyo ili kutoa fursa kwa Watanzania watakaohitaji kuchanjwa kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19 waweze kuipata kwa ukaribu na urahisi zaidi na si vinginevyo.
 
C muambiane ktk chama lenu chakavu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, Serikali haitamlazimisha mwananchi kuchanjwa chanjo ya corona. Amewataka Watanzania wapuuze upotoshaji unaosambazwa “Chanjo ni hiari tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake."
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, Serikali haitamlazimisha mwananchi kuchanjwa chanjo ya corona. Amewataka Watanzania wapuuze upotoshaji unaosambazwa “Chanjo ni hiari tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake."
Huyu mzee hata kuongea hajui
 
Kwani sisi tumesema huo mpango umeandaliwa na serikali, au mabeberu? nyinyi ni wademkaji tu wa ngoma ya mabeberu....maswala ambayo yanatakiwa yafanywe na watafiti kama kutoa maelezo toshelezi kuhusu hayo majaribio ya chanjo kabla ya kuomba ridhaa kwa watu, nyinyi ndo mnaonekana mpo front kuyafanya, halafu mwishoni mnaruka kimanga kwamba hamtahusika na madhara yoyote yatakayojitokeza...
 
Wiki yote iliyopita iligubikwa na maagizo mbambali ya kujikinga na ugonjwa hewa wa corona Tanzania.
Yani ugonjwa wa corona unatafutwa kwa tochi nchini Tanzania.

Dunia inakotoka sisi watanzania ndiyo tunaenda kwa kasi ya 4G!!
Dunia nzima wanaachana na mashariti ya distance na barakoa sisi ndiyo imegeuka wimbo ,hadi watoto wa shule za msingi huko vijijini wanalazimishwa wavae barakoa!

Hivi corona ingeingia mwaka 2019 tukiwa na viongozi wa aina hii ,hali ingekuwaje?
Hata hivyo wananchi wameamka na kupuuza maagizo yote na wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
 
Kumekucha Salama
Hoja Ya Nguvu
Nguvu Ya Hoja

Che~Che Zinatoka Sasa Hivi
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, Serikali haitamlazimisha mwananchi kuchanjwa chanjo ya corona. Amewataka Watanzania wapuuze upotoshaji unaosambazwa “Chanjo ni hiari tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake."
Lakini inaweza kuwatwanga raia wake risasi, kuwapoteza na kuwabambikia kesi za uongo? Kilangila.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, Serikali haitamlazimisha mwananchi kuchanjwa chanjo ya corona. Amewataka Watanzania wapuuze upotoshaji unaosambazwa “Chanjo ni hiari tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake."
Tunamsikiliza ASKOFU GWAJIMA

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Sina hakika kama Gwajima angekua ni mwana chama wa Chadema baada ya mahubiri yale saa hzi angekua wapi, again sina hakika kama maneno yale yale au mahubiri yale yale yangetamkwa/yangehubiriwa na mwana chama wa Chadema au askofu Mwamakusa, sasa hvi angekua wapi? Huenda angekua na kesi ya uchochezi, anyway labda ni mawazo yangu tu
 
Gwajima ndio mkweli.wengine ni wajasiliasayansi
No na gwajima. Sauti nyika
 
CCM Ni ile ile Cha msingi Ni sisi watz kujitambua
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, Serikali haitamlazimisha mwananchi kuchanjwa chanjo ya corona. Amewataka Watanzania wapuuze upotoshaji unaosambazwa “Chanjo ni hiari tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake."
Tatizo ni wale wataalamu uchwara ili kulinda ugali hupotosha,na kiongozi mwenyewe huamua kupotea Bila kupotoshwa wakati mwingine.
Tunachotaka ni elimu tu pande zote wanaoziamini na wasioziamini chanjo watoe ya moyoni,wananchi tutaamua.
 
Back
Top Bottom