Waziri Mkuu, unda tume kuchunguza NBAA!

Hujui Hujui tu iko siku utashindwa kupanda Mtungi uite balozi achunguze chumba chako. Hahahaaaaaa CPA ni wa WAHASIBU sio JANJAJANJA.
 

Dogo usijigambe kabla hujavuka mto wenye mamba wengi unaweza ukashindwa kuliondoa hilo somo moja lililobakia hadi wakakufutia module F nzima kwani kuna wengi yaliwakumba.Mtoa mada ana jambo la msingi.
 
MHASIBU HALISI mimi nakubaliana wewe hiyo tume uindwe lakini si kuchunguza ufaulu kiduchu bali wachunguze kwa nini wahitimu wa CPA wa siku hizi ukimpa trial balance hawezi kuandaa final accounts kama wahitimu wa miaka 90s?
 
Last edited by a moderator:
MHASIBU HALISI wewe ni muhanga wa shule ya uhasibu na ukaguzi.wengine tulikwisha maliza tunakula good time mitaani.wewe endelea kulia tu na machozi yako yanaenda na MAJI.SUBIRI SYLABUS MPYA ya kurekodi somo moja unaweza kubahatisha nawe ukapat GA.

Kama ulikwisha maliza na kupata CPA, juzi ulikuwa unalia lia nini na Bwana Daudi? Nilikwambia niPM nikupe michongo ya mjini
 
MHASIBU HALISI inakuwaje anashindwa kupata CPA, ni kwa nini usiwe miongoni mwa hao 300 na kuwa kati ya 2700? Unajua nchi hii inaelekea idadi ya wajinga tu wengi na hata wanaopass inawezekana 80% bado wanatumia ujanja.
Kama hali si hali kajaribu professional nyingine na sio uhasibu tu. Nenda kasome pale Ustawi wa Jamii Bamaga au Kivukoni
 
Kupata CPA lazima ufanye juhudi au uwe na nature, sio lele mama. Wanaolalamika wamezoea vyuoni wanakopata course work marks za bure, kutumia vibomu (phantom), cheating, mara area of concentration nk. Masomo ya CPA ni hayo hayo yanayofundishwa vyuoni na wakati mingine mitihani inafanana na ya vyuoni. NBAA hakuna kuhonga pesa, wala penzi au undugu. Na kama vyuo vyote vingetumia system ya NBAA tungekuwa na wahitimu halisi sio hawa ambao baadhi ni feki, halafu wanalalamika oooh eti wageni wanaajiriwa badala ya wazawa.

Iliwahi kutokea chuo fulani karibu wanafunzi wote wa kozi moja walifeli, wakatoa malalamiko, yule mwalimu aliitwa na utawala kwa nini ilikuwa hivyo, mwalimu akawaita wanafunzi ni eneo gani au kitu gani kilitahiniwa na hakuwafundisha wakabaki wanang'aa macho. Hata hivyo yule mwalimu alionywa eti atasababisha chuo kukosa wanafunzi maana wakifeli sana wataogopa kujiunga watapata hasara. Ndio maana siku hizi Disko (Discontinue) zimepungua sana. Hii ndio elimu yetu na si ajabu unakuta darasa la saba hajui kusoma na kuandika halafu mnataka apate CPA!!!.

Jitahidi mwanangu kwani hao wanaofaulu ni Miungu, kwa nini wewe usifaulu??
 
wa tanzania bwana kwa kupenda vimtelemko,acha kunung'unika wewe,naona jasho mpaka kwenye meno.mim naona ni sawa sawa,and i believ the tougher the exams the more u need excellnc preparation and deeper knowledge,na ndio maana watu kama wewe ni lazima uchujwe becoz huna vigezo vya kuperfom
 
"mtu dhaifu na mwazo dhaifu ....." shida ni NBAA au vyuo tulivyosoma na GPA za kedesa?
 
nbaa wapo sawa maybe ni kucheck sylabus ichange masomo yawe mengi watu wawe wakifaulu moja ndo basi.otherwise keep it up bodi.nategemea soon ntakuwa kwenye list yenu.
 
Mhasibuhalisi,tatizo kubwa tunalokutana nalo wahasibu ni kusoma umetoka kazini na la pili anayetunga mtihani siye aliyekufundisha,hapo ndipo kazi ilipo.Na ukitoka kazini umechoka sana lakini inabidi ufungue japo kitabu upitishe macho.Wote tumepitia huko kaza uzi utafanikiwa tu,nina uhakika utavuna mbivu safari hii usikate tamaa.Na ni ukweli kabisa bila CPA(T) bado hujawa muhasibu.PIga shule mbivu zinakuja.
 

nitakutumia PM ili tushauriane kamanda
 
Last edited by a moderator:
hii thread!nimesoma comments zote nikaamua nami nichangie kidogo kwani namimi naendana na fani kidogo
  • kwanza wanataaluma tunashida katika maandalizi ya mitihani,Wengi wanaosoma hawapati muda wa maandalizi ya mtihani ,bodi inashauri tufanye maandalizi sio chini ya miezi tisa kabla ya kufanya mtihani lakini chaajabu sisi tunasoma miezi 4 alafu tunataka kufauli hili jambo aliwezekani hata kidogo,kama ukifanikiwa basi utakuta ulimeza swali la ACCA ukalikuta kwenye mtihani
  • syllabus ya NBAA haimjengi mwanafunzi kuelewa ndio maana wanataka kubadilisha iwe ya competent based education kutoka katika knowledge based!ndio maana leo wahasibu wakitanzania kunavitu fulani tunashindwa kuvifanya tunapo kabidhiwa Multinational company kuziongoza,ata huku kwenye utumishi wa umma mtu akipata CPA anapandishwa cheo anakuwa kazi kubwa nikuwa muidhinishaji na sio mtendaji ukimpeleka kwenye taasisi zenye challenge anashindwa kuperform
  • kuibuka kwa vyuo kama uyoga vinavyotoa elimu ya uhasibu bila ya kuwa na wataalamu wa kutosha wakutoa hiyo elimu.mfano mzuri chuo nilicho soma zile core subject za accounts nilifundishwa na PHD holders ambao hawana CPA, sasa kama hali ni hiyo kwa chuo changu chenye umri karibu na nusu karne habari gani kwa vyuo vyenye miaka chini ya 5,na hapo tunategemea kwelui matokeo ya NBAA yawe mazuri?
  • kusoma kwa kuiga kuanzia miaka ya karibuni kumeibuka na wimbi la watu kupenda kusoma course ya accountancy kwakuwa waliona fulani kasoma na maisha yamekuwea mazuri,nakumbuka miaka iliyopita niliwahi kutoa hii comments enzi hizo nilikuwa na tumia ID nyingine hapa JF ,watu walinitukana sana kwa hiyo comments ambayo niliwaambia wahasibu wengi ,sio wanataaluma wakweli walifuata taaluma baada ya kuwaona wakina fulani maisha ni mazuri!uhasibu haupo moyoni ndio maana kujituma kupata CPA wanaona kazi sana
  • mwisho kwa ushauri kama unaona mitihani ya NBAA inakusumbua jaribu kufanya CISA au CIA ni mitihani mizuri na upesi kufaulu na international recognized
 

Mtoa mada, kama huna CPA kama ulivyosema kwenye post yako unapaswa kubadili jina. Jiite karani wa uhasibu.
Pia nakushauli uongeza bidii kwenye kusoma. Jitahidi uwe unaelewa kwani NBAA hamna semina questions kama ulivyozoeshwa na walimu wako vya vyuo na pia hamna marks za group assignment. Mimi nilianza kusoma na wenzangu kama 10, wote tulishamaliza in less than two years.
 

Hongera!
 

Pole sana!!!!! Halafu ni jinsi gani unaonesha ulivyo mtu wa kukariri..... Hufikirii kitaalamu kama inavyotakiwa kuwa maana hata ku quote umechukuwa kakipande ka hoja nzima tu na kisha kuhitimisha kama ulivyosoma tunotisi twako twa chuo ukafaulu kwa kubahatishabahatisha tu. Kufanya mitihani mara mbili si kigezo cha ubora wa NBAA!!! Tunazungumzia professional nzima ya namna ya uendeshaji NBAA na mitihani yake kwa ujumla. Kwani kazi ya NBAA ni kutunga mitihani tu? Hebu soma comments zangu hapo juu (na si ku quote kamstari kamoja) utagundua hata ICAEW ambao ni wasomi kupita wewe uliyepata CPA kwa sitting mbili wanasemaje. Au hujaielewa??? Kama hujaelewa soma tena comments zao (zingine).

The current syllabus​
We recognise that the current professional syllabus has served well, despite the low pass rates in final examinations. During stakeholder discussions almost every NBAA member emphasised that quality standards must not be lowered to achieve improvements in pass rates.
The syllabus is, at a point, in its life cycle. However, where it needs to be considered, challenged and refreshed. The syllabus content and articulation is one key driver of the approaches used and, therefore, the effectiveness of teaching and learning. The teaching and learning model that NBAA syllabus currently supports includes provision of fulltime education from institutions that enable students to gain exemptions from the Foundation and Intermediate stages of the Professional qualification. Such institutions educate a large proportion of
undergraduates who then pass on after graduation to take their NBAA Final Stage examinations. The NBAA professional examinations at Foundation and Intermediate stage are only taken by around 100 candidates at each sitting. The Final Stage Module E exams are taken, including candidates retaking exams, by around 2,000 candidates. The Final Stage Module F exams are only sat by around 800 Candidates.
Both the Final Stage exams have pass rates around 20%. The lower level NBAA exams have pass rates around 40%. The Final Stage tuition is almost always undertaken using part-time classes, often evening classes supported by a few days of review classes. Clearly, many candidates coming through the various exempting routes are falling short of the professional examination standards and many students are not coping with the current examinations purely based on teaching and learning from their part-time classes and diverse study materials.
We believe that the low pass rates are in part due to the scale, scope, content, specification and nature of the existing syllabus and related learning materials.

The current assessmentsThe NBAA currently assesses students based on centrally-set unseen three hour examinations that are held twice a year in November and May.Students who attend an approved institution may receive exemptions from all, but the Final Modules E and F.Several stakeholders expressed concerns that the standard of teaching and learning, the levels of assessment applied and the quality and qualities of the population of exempt students was falling below the professional requirement and may be contributing to the low pass rates. Overall, the pass rate at the Final Module level is around 20%.A team of examiners are used to provide papers that are moderated by the NBAA. The papers created by examiners are generally broken down into questions that may be assembled by the NBAA to create an exam for a particular sitting. The examiners, who may also teach the NBAA students, are, therefore, not in a position to know the content of an exam paper in its entirety before it is sat. This may, however, give rise to inconsistent examination of core topics over time and to a lack of consistent adherence to syllabus weightings.Specific observationsWe have not made specific observations on individual exam papers but would be happy to discuss such matters if required to enhance understanding of the observations above.Although the observations above should be seen as matters that should be dealt with by the NBAA through required improvement steps it must be borne in mind that such development needs would emerge even in some of the best bodies around the world.The current examination paper assessments have considerable strengths but as with the syllabus content from which they are derived they are more academic than practical, are not always totally clear in specification and requirement and are not sufficiently consistent in balance and in examining core competences with a focus on the knowledge, skills and application required of an accounting professional.
UNAONA??????? Wadau wengi wanalalamika na MHASIBU HALISI pekee. Hata ICAEW wanakiri hivyo lakini wewe unaona sawa tu kisa ulifaulu CPA kwa kufanya sitting mbili!!!!!! Pole sana........ Tatizo walilolieleza wenzio soma alama za blue nilizokuwekea tatizo ambalo wewe hulioni bali unaona kufaulu kwa sittinh mbili ndo ufahari.
 
Pole sana kwa bidii utafanikiwa!
 
CPA sio lelemama,kama wewe ni bongo lala tafuta fani ingine!
 
Makarani kwa kulalamika bana!!!

angalia rate za ufaulu ACCA,CPA(K),CPA-USA,CPA-CANADA bado rate za ufaulu ni ndogo na % of difference with CPA(T) si kubwa sana pia!

Maisha si lelemama bana!
 
NBAA ina mapungufu mengi mno ambayo hayajaandikwa hapa! Ndio maana ma donor kupitia BOT wakataka restructuring of NBAA ili wawe na uhakika na fund zao zinazomwagwa Tz!

Kuna changes nyingi za kufanywa ingawa upinzani mkubwa ni wahasibu wakongwe ma conservative like Yona Killaghane wasiopenda sana mapendekezo ya wazungu likiwemo la sifa za Executive Director wa NBAA ambalo ingefanya awekwe mtu wanaomtaka wao!

Kenya ACCA ina nguvu sana kuliko CPA(K) mnajua sababu?
 
Nadhani mpaka utoe rushwa ndio unapewa cpa. Ukisoma MBA na wenye cpa utashangaa wengi wako kaputi na hawamalizi. Sawa kabisa mkuu, iundwe tume huko kuna urasimu wa ovyo kabisa.

MBA hii hii ambayo iko kama njugu au ni MBA gani hiyo inayowakimbiza wahasibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…