Mzalendo JR
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,193
- 515
Hujui Hujui tu iko siku utashindwa kupanda Mtungi uite balozi achunguze chumba chako. Hahahaaaaaa CPA ni wa WAHASIBU sio JANJAJANJA.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa upande wangu naiunga mkono NBAA kwa kuhakikisha inatoa watu ambao ni professional,mimi namalizia somo moja la Module F kwa sasa hivi.Kwa kweli mitahani yake inahitaji
maandalizi ya kutosha na uhakika.Aliyetoa mada hii inaonekana ni mtu aliyejaribu kuifanya hii mitihani akashindwa, na naona alidhani ni mteremko,hivi ndo tunataka bodi iwe.Kama umeshindwa nenda masters au kwenye bodi nyingine, hatutaki vihiyo.
MHASIBU HALISI wewe ni muhanga wa shule ya uhasibu na ukaguzi.wengine tulikwisha maliza tunakula good time mitaani.wewe endelea kulia tu na machozi yako yanaenda na MAJI.SUBIRI SYLABUS MPYA ya kurekodi somo moja unaweza kubahatisha nawe ukapat GA.
Wale jamaa wa NBAA nakumbuka walinikamata mara moja tu kwenye Auditing & Investigation. Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufanya Supplimentary exam kwenye historia yangu ya shule. Usema kweli ile mitihani yao si ya kujenga taaluma bali ya kukomoana. After all they are just copying from ACCA past papers.
TUMBIRI (PhD In Progress, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd [/SUP]Overall Best Student in Form Six National Exams),
tumbiri@jamiiforums.com
Nakala: MHASIBU HALISI, Kimbunga, etc
Ni hivi majuzi tu Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda aliunda tume kuchunguza sababu za kufeli kwa wanafunzi wa Form Four iliyopelekea kuwa na matokeo mabaya nchi nzima.
Tunakuomba Mheshimiwa Waziri Mkuu kuunda tume nyingine ili kuchunguza kuwepo kwa matokeo mabovu kila mwaka kwa miaka nenda rudi kwa watahiniwa wa mitihani ya CPA (Certified Public Accountant) inayotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa mahesabu (NBAA).
Tunasema kuna umuhimu wa kuunda tume kuchunguza bodi hii kutokana na ukweli kwamba mitihani inayotolewa na bodi hii ni ya kukomoana sana.Lengo lao ni kuhakikisha kwamba wanaopata hiyo CPA wawe wachache mno. Kwa mfano wanaweza wakafanya mitihani hiyo watahiniwa zaidi ya elfu tatu (3,000) lakini watakaopata hiyo CPA ni chini ya watahiniwa mia tatu tu (300).
Sisi wahasibu tunaona bodi hii haikuundwa kuendeleza taaluma hii ya uhasibu bali ni kuididimiza taaluma hii ili kuwe na wahasibu wachache mno wenye sifa za kuitwa wahasibu. Kwa sababu kwa mujibu wa Ndugu Ludovick Utouh ambae ni mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) anamtambua mhasibu ni yule mwenye CPA tu. Hawa wengine wanaofanya kazi za uhasibu lakini hawana CPA wanajipendekeza tu na ndio wanaoharibu kazi na sifa za taaluma ya uhasibu.
Bodi hii ya NBAA imejihakikishia maisha ya kifahari kwa kila mtumishi wake kutokana na kukusanya mabilioni ya pesa ya bure kutoka kwa watahiniwa wa mitihani yake.
Kwa mfano hii sheria waliyoiweka ya kwamba Mtahiniwa akifanya mitihani na kufaulu somo moja basi wanalifuta, ni sheria kandamizi yenye lengo la kuwarudisha nyuma watu wanaopenda kujiendeleza katika fani hii na vile vile kuleta aina mpya ya UTUMWA kupitia sekta ya elimu. Yaani mtu atumie robo tatu ya umri wake wa kufanya kazi akiwa anasoma.
Sisi binafsi(Wahasibu) hatuelewi kama mtu somo amefaulu eti kwa kuwa ni moja linafutwa kwa nini ? Wakati mpaka huyo mtu amelifaulu hilo somo ametumia rasirimali chungu nzima ikiwemo Muda,Fedha na Jitihada kubwa mpaka kufaulu somo hilo. Imefikia mahala waajiri wengi hawataki kuwalipia wala kuwaruhusu wafanyakazi wao kufanya mitihani hii kwa kuwa wameona ni kupoteza muda na rasilimali tu. Mtu badala ya kutumia muda wake mwingi katika kufanya kazi ili kuinua uchumi wa taifa, badala yake anatumia muda mwingi kusomea CPA ambayo kuipata kwake ni mpaka Mabwana wakubwa wa NBAA watakapokuwa tayari kukupa. Tunasikitika sana kuona nchi kama ya Uingereza ambayo imetuacha mbali mno kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla, ukifanya mitihani yao ya ACCA hata kama ni somo moja moja na ukafulu wanali-record na unamalizia mengine yaliyobaki. Lakini kwa NBAA ukifaulu somo moja wanalifuta.
Kwa kumalizia tunakuomba Mheshimiwa Waziri mkuu, usisubiri mpaka kutokee maandamano unda tume kuchunguza utendaji kazi wa Bodi ya NBAA kwani imekithiri kwa kufelisha watahiniwa wake kwa makusudi.
Wale jamaa wa NBAA nakumbuka walinikamata mara moja tu kwenye Auditing & Investigation. Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufanya Supplimentary exam kwenye historia yangu ya shule. Usema kweli ile mitihani yao si ya kujenga taaluma bali ya kukomoana. After all they are just copying from ACCA past papers.
TUMBIRI (PhD In Progress, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd [/SUP]Overall Best Student in Form Six National Exams),
tumbiri@jamiiforums.com
Nakala: MHASIBU HALISI, Kimbunga, etc
MOSI. Je unaunga mkono hoja ya huyu kilaza ya Waziri Mkuu kuunda Tume?
PILI. Uhasibu siyo ELIMU bali ni FANI kama zilivyo fani za uhandisi, wakili, daktari n.k. Kufeli mitihani ya NBAA ni kukosa msingi imara wa elimu yetu ya juu maana kwanza NBAA haifundishi bali ina 'test' uelewa wa ulichojifunza kwenye elimu yako ya juu. Ndiyo maana aliyemaliza shahada ya uhasibu au advanced diploma ya uhasibu anasamehewa baadhi ya masomo kwa assumption kuwa hayo aliyosamehewa anayafahamu maana alishajifunza. Ambaye akusoma uhasibu kwenye shahada yake hapati msamaha kwa kuwa wanajua hakusoma hivyo inabidi asome.
Kwani huko vyuoni wote wanafaulu kuhalali? Ndo hao hao wanaingia kufanya mitihani ya CPA. NBAA watu wanakwama kwa sababu HAWAHONGEKI. Mbona mimi nimefanya mitihani bila hata kuhudhuria hizi mnaita review classes. Nimetumia notisi zangu na elimu ya chuo na nikafaulu tena kwa sitting mbili tu. Tuache kuhamisha matatizo wakati sisi wenyewe ndo tuna matatizo
Nadhani mpaka utoe rushwa ndio unapewa cpa. Ukisoma MBA na wenye cpa utashangaa wengi wako kaputi na hawamalizi. Sawa kabisa mkuu, iundwe tume huko kuna urasimu wa ovyo kabisa.