Waziri Mkuu, unda tume kuchunguza NBAA!

Waziri Mkuu, unda tume kuchunguza NBAA!

MHASIBU HALISI kiwango kidogo cha ufaulu wa CPA(T) kinatokana na sababu zilizotajwa na wadau zikiwemo kutokuwepo course work,watahiniwa wengi wanafanya mitihani hiyo wakitokea kazini,integrity ya staff wa NBAA na nyinginezo nyingi.Pia hata ukichunguza ufaulu wa bodi nyingine kama ACCA,CIMA,CIA,CFA,CISA bado upo chini sana.
Usife moyo kaza buti ili ukaribie kwenye u-professional accountants.


Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Pole sana!!!!! Halafu ni jinsi gani unaonesha ulivyo mtu wa kukariri..... Hufikirii kitaalamu kama inavyotakiwa kuwa maana hata ku quote umechukuwa kakipande ka hoja nzima tu na kisha kuhitimisha kama ulivyosoma tunotisi twako twa chuo ukafaulu kwa kubahatishabahatisha tu. Kufanya mitihani mara mbili si kigezo cha ubora wa NBAA!!! Tunazungumzia professional nzima ya namna ya uendeshaji NBAA na mitihani yake kwa ujumla. Kwani kazi ya NBAA ni kutunga mitihani tu? Hebu soma comments zangu hapo juu (na si ku quote kamstari kamoja) utagundua hata ICAEW ambao ni wasomi kupita wewe uliyepata CPA kwa sitting mbili wanasemaje. Au hujaielewa??? Kama hujaelewa soma tena comments zao (zingine).


Ni quote lote la nini sasa wakati huna issue. Kama vipi nenda kafanye mitihani ya ACCA
 
Kama ulikwisha maliza na kupata CPA, juzi ulikuwa unalia lia nini na Bwana Daudi? Nilikwambia niPM nikupe michongo ya mjini

SEBM umenivunja mbavu, nilikwisha sahau timbwili lile la PSRS nilivyokukomalia juu ya kuwatetea.NitakuPM mkuu
 
Last edited by a moderator:
wajinga ndio wanadhani CPA ndio maisha, wajinga ndio wanaringia CPA huku wakipewa wasolve real accounting problems wanashindwa. nina bcom yangu nzuri ya acc nafikiri nahitaji kuendelea kufanya kazi kwa muda nipate uzoefu huku nikipata mshahra mzuri tu, nikitaka kujiendeleza nitasoma MBA na sio CPA ya kupoteza muda na pesa, ndugu jipange, hujasoma mpaka chuo kikuu uje ulalamikie mabwana wa NBAA. Kuna wahitimu kibao wamepata kazi za uhasibu na wanafanya kazi vizuri bila hata ya hizo CPA, usifanye CPA wa determine future yako.
Endelea kujilisha upepo na utagundua kumekucha.Mawazo yako ni finyu na umesoma accounting kwa bahati mbaya tu.Wengi waliosoma Accounting na wanafikria mbele siyo kuajiriwa na kulipwa mishahara mizuri la asha bali na wenyewe baada ya muda kuajiri watanzania kwa kuanzisha Auditing firms zao baada ya Muda.Bila kuwa na CPA hata ufanye kazi miaka kibao uwezi pewa leseni ya kupractice ACAPP.Kuna vijana walimaliza CPA na sasa wanafirm zao wanapiga mziko kwa kwenda mbele.Jiandae kuendelea kuwa Karani ndugu yangu.
 
[/FONT][/COLOR][/LEFT]
[/COLOR][/SIZE][/FONT][/COLOR][/SIZE][/FONT][/COLOR][/SIZE][/FONT]
Ni quote lote la nini sasa wakati huna issue. Kama vipi nenda kafanye mitihani ya ACCA

Nilijua tu utaishia kutukana maana mapolisi huwa hawana akili....... Fikiria selection zote za waliofaulu zikiisha ndo waliobaki wanakwenda polisi. Hii ni baada ya waalimu kuchukuliwa ndipo na mapolisi wanachukuliwa. Wewe unafikiri hao polisi wanaochukuliwa baada ya selection zooote hizo watakuwa wana division gani?
 
CPA ni professional qualification, lazima iwe awarded kweli kwa watu wenye ujuzi na uelewa wa mambo ya uhasibu na related subjects, ni watu tunaowategemea kufanya financial decision serikalini na kwenye sector binafsi. Kwa kuwa na cheti cha CPA maana yake tunaweza kukuamini na kukupa nafasi ya juu tukitegemea kwamba una ujuzi wa kutosha katika taaluma ya uhasibu. Kwa msingi huu, hoja si wingi wa watu wanaofaulu mitihani ya CPA, hoja iwe ni ubora wa wale wanaofaulu ili wawe na uwezo wa kufanya kazi ya uhasibu kwa ufanisi unaotakiwa.

Leo kuna vijana wanamaliza degree za uhasibu tena wengine wanamaliza na MBA kabisa lakini ukikutana nao kwenye intavyuu ndiyo utashangaa, maana wako empty kabisa, na hao wakigusa tu NBAA lazima 'waliwe vichwa', wengine ndiyo kama hawa wanakuja huku kulalamika. Sasa fikiria kama NBAA na wenyewe wasingekuwa makini kama ilivyo kwa vyuo vyetu vingi, ungeweza ukakuta kijana ana BCOM, MBA na CPA lakini ukimpiga intavyuu anakuwa hana tofauti sana na ile 60% ya mtihani wa form 4 wa mwaka jana, yaani zero kabisa.

Ni ukweli usiopingika kuwa asilimia kubwa ya wahasibu wana aspire kuwa na CPA, lakini angalia wale wanaozipata, ni wale ambao walikuwa na uwezo mzuri toka wakiwa chuo na hata GPA zao za chuo ni nzuri, lakini kama wewe ni kilaza kiukweli itakuchukua decades kufaulu mitihani ya NBAA, by the way vilaza wengi wakijaribu mara moja wakimatwa hawarudi tena na ndiyo hao wanaoanzisha propaganda eti CPA ya nini wakati naweza kufanya kazi vizuri tu na degree yangu. Hakuna mtu asiependa recognization, CPA above all it brings your recognization as professional Accountant, kwa hiyo walioshindwa mitihani ya NBAA ni bora wakawa wakweli kwa kusema wameshindwa badala ya kusema ya nini.
 
inaonekana we ni msomi lakini bado ni mtumwa wa usomi wako, nani kakwambia lazima niwe practising accountant? wakati nimegundua field nyingine katika business na commerce kwa ujumla ambazo ni more exciting na challenging na zina-mpa mtu upeo mpana zaidi kuliko hiyo mitihani ya CPA.
sijasoma mpaka chuo kikuu ili niendelee kuwa mtumwa wa wasomi wenzangu, kama wewe ulivyo.
 
:nono:mtu anaposema CPA ya nini ni Ishara mojawapo kuwa anajiamini anaweza kufanikiwa katika lolote analolifanya bila ya kuwa na CPA, EITHER KAZI YA UHASIBU OR BUSINESS RELATED BILA YA KUWA NA HIYO CPA, KWA HIYO AMEAMUA KU-MOVE ON SABABU AMEONA CPA ITAMPOTEZEA MUDA NA WAKATI. MTU WA AINA HII NAMPONGEZA SANA COZ AMEAMUA KUTOKUA MTUMWA WA WASOMI WENZIE(NBAA)
 
Najipanga kuchukua CPA Baada ya miaka 4. Ryt now najipanga.
"if its hard, go harder"
mtoto akifail wazazi wanamkalisha chini.
MZAZI AKIFAIL???
Ukifail kupata CPA Tambua kwamba bado haujaiva kuwa mmiliki. Chakufanya ni kujipanga ili uipate na si kulalamika.
"I think u can get it if u want it coz what others done to deserve & secure it"

"IT CAN BE DONE,PLAY UR PART"
 
I will say something that will shock you, CPA ya Tanzania is the easy compared to many certified exams hapa duniani such as CFA. Problem ni kwamba most of CPA question Kwa Tanzania ni irrelevant sababu people don't use. I will give you example codification for options evaluation. This is total irrelevant sababu Tanzania companies doesn't even issue options.

Things like consolidation, system audit all this are just rocket science Kwa normal accounting graduate. Only section ambayo inaweza kusumbua ni tax sababu Tanzania code is a complicated code on earth. Other than that CPA ya bongo no chai.
 
MHASIBU HALISI wewe ni muhanga wa shule ya uhasibu na ukaguzi.wengine tulikwisha maliza tunakula good time mitaani.wewe endelea kulia tu na machozi yako yanaenda na MAJI.SUBIRI SYLABUS MPYA ya kurekodi somo moja unaweza kubahatisha nawe ukapat GA.

Duh umempiga rungu la kichwa! NBAA bwana usipokaa vizuri wanakula kichwa! Kuna watu wamesoma miaka na mikaka lakini hawainusi hiyo kitu inayoitwa CPA!

Ila hii ni mitihani ya kitaaluma hivyo ni jukumu la wanataaluma kuliangalia suala hili kwa umakini japo inajulikan wazi kwamba watu huwa hawajitayarishi vyema kabla ya mitihani. Sasa hivi Ludovick Uttoh ameanzisha darasa pale Msimbazi Centre ili kuwasomesha wakaguzi wa ofisi ya CAG. Vijana wanalipiwa wanafanya review ya nguvu naona wanafaulu wengi.
MHASIBU HALISI jipange utaupata uhasibu
 
Last edited by a moderator:
NBAA ni bodi ya ukweli ya uhasibu Tanzania hiyo sio NECTA bwana hyo ni bodi inayotoa cream tupu kama ww ni kilaza huna lako hapo katafute nazi ukune

atoe hongo kama anaweza chezea cpa weyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Sasa mbona mnamu attack yeye kama yeye.

Mashambulizi yenu myaelekeze kwenye hoja yake sio mtu binafsi.
 
Lol..eti Pinda achunguze?why Pinda na kwa utaalam gani au authority gani juu ya hizi bodi au kwa sababu ni PM?nafikiri TZ kuna bodies zinazo regulate na kusimamia hizi professional/academic institution ungeanzia huko kuliko kuleta politics za kina Pinda,wasomi wanachukia sana kuingiliwa na know nothing politicians.
 
Chuo si mnadesa! Mnadhani CPA kudesa kama chuo? Wengine vyuoni mnvua c....pi ili mpate degree.
 
Kupata CPA lazima ufanye juhudi au uwe na nature, sio lele mama. Wanaolalamika wamezoea vyuoni wanakopata course work marks za bure, kutumia vibomu (phantom), cheating, mara area of concentration nk. Masomo ya CPA ni hayo hayo yanayofundishwa vyuoni na wakati mingine mitihani inafanana na ya vyuoni. NBAA hakuna kuhonga pesa, wala penzi au undugu. Na kama vyuo vyote vingetumia system ya NBAA tungekuwa na wahitimu halisi sio hawa ambao baadhi ni feki, halafu wanalalamika oooh eti wageni wanaajiriwa badala ya wazawa.

Iliwahi kutokea chuo fulani karibu wanafunzi wote wa kozi moja walifeli, wakatoa malalamiko, yule mwalimu aliitwa na utawala kwa nini ilikuwa hivyo, mwalimu akawaita wanafunzi ni eneo gani au kitu gani kilitahiniwa na hakuwafundisha wakabaki wanang'aa macho. Hata hivyo yule mwalimu alionywa eti atasababisha chuo kukosa wanafunzi maana wakifeli sana wataogopa kujiunga watapata hasara. Ndio maana siku hizi Disko (Discontinue) zimepungua sana. Hii ndio elimu yetu na si ajabu unakuta darasa la saba hajui kusoma na kuandika halafu mnataka apate CPA!!!.

Jitahidi mwanangu kwani hao wanaofaulu ni Miungu, kwa nini wewe usifaulu??

Unajua mzeelapa majibu yako yamenifanya niangalie hii issue kivingine kabisa. Nimelinganisha accounting profession na profession nyingine nimeona kwamba accounting is the only profession inayodiscourage watu kwenda University. Yaani wakati sijaona MaEngineer, MaSosholojist, MaLawyer nk sijawahi kuona wakikandia degree zao za vyuo vikuu fani ya uhasibu pekee ambayo hukandia degree za vyuo vikuu. Sasa kama hizo degree za uhasibu (Bachelor hadi Masters) hazina maana kwa nini vyuo vikuu vinaendelea kuzitoa, na kwa nini serikali ilipie huko na isiwalipe NBAA na waconduct hizo classes. Kwa maneno mengine serikali iondoe degree za uhasibu kwenye vyuo vikuu na kuwapa NBAA mandate ya kuandaa wahasibu na pesa yote ilipwe huko.

Nachokisema hapa unaweza kulinganisha na hii story kwenye the guardian ya Uingereza.

Lawyers and accountants need not have degrees, says minister
Accountancy and legal firms join £25m trial of plan offering apprenticeships
C:\Users\Challu\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.jpg

Balfour Beatty is among the companies providing new qualifications for their apprentices. Photograph: Cate Gillon/Getty Images
The government has announced plans to allow school leavers to become lawyers and accountants without first gaining degrees. Matthew Hancock, the minister for skills, said he wanted to expand the apprenticeship scheme to offer qualifications at the same level as a master's degree without years of university study.
"At the moment, to become qualified as a solicitor, accountant or in insurance, the typical route involves three years at university, then on the job training and professional qualifications. But university is not for everyone. There is no reason why you can't attain the same qualifications, without the degree, starting on the job training in an apprenticeship from day one," he wrote in an article in the Daily Telegraph. "So I want apprenticeships spanning craft, technical and professional jobs that open up work-based routes to the top."
The government has funded around 30 employers, including the accountancy firm PwC and construction company Balfour Beatty, with £25m to provide new qualifications for their apprentices.
At present apprentices can reach the level of a foundation degree after four years. The Department for Business, Innovation & Skills announcement envisages apprentices continuing study for up to eight years to attain the equivalent of a master's degree.
Hancock wrote: "There are successful higher apprenticeship schemes already in place, at levels four and five, equivalent to the first year of a degree course and foundation degree levels respectively. I now want to see more courses that truly match graduate and postgraduate qualifications.
"From next year, apprenticeships at levels six and seven – bachelor's and master's degree level – will be officially recognised for the first time."
Student numbers in England and Wales have fallen by 57,000 in the last year largely because of the increase in tuition fees. The apprentice scheme will allow some school leavers to work and study at the same time, if an employer is willing to fund it. "Higher apprenticeships, like all apprenticeships, are employer-led. So to ensure their success and go further, we need more employers to step up to take advantage of the opportunity," said Hancock. The minister said Britain's economic progress has been slowed by a lack of respect for learning in the workplace. "For decades, Britain has been held back by artificial and counter-productive divisions between practical and academic learning, allowing countries such as Germany to get ahead in the global race for technical excellence," he said.
The government's announcement was inspired by a report this year by Doug Richards, a businessman who appears in the television show Dragons' Den. Richards told the government that apprenticeships should have parity with degrees.
The government is in talks with the BPP Law School over an apprenticeship that will lead to a qualification as a solicitor and PricewaterhouseCoopers is developing a master's-level apprenticeship for a qualification in audit, accountancy or tax, Hancock wrote.

Chanzo: http://www.guardian.co.uk/education/2012/dec/28/lawyers-accountants-need-not-have-degrees
 
Tangu NBAA ianzishwe mwaka 1972 walioipata hiyo CPA hawazidi watu 4,500 . Wakati huohuo mahitaji ya watu wenye CPA katika soko ni karibu watu 10,000 mpaka sasa.

Katika idadi hiyo ya wahasibu 4,500 si kweli kwamba wote wanaishi mpaka hivi leo. Mungu hakusema kwamba ukiwa na CPA basi hutokufa. kwa hiyo kuna ambao wameipata hiyo CPA laikini tayari wameshakufa. Tena waliozipata hizo CPA na wakawa hawana maadili ya maisha , wanakufa haraka sana kuliko hao ambao hawana hiyo CPA. Kwa hiyo basi " Kazi nyingi za uhasibu zinafanywa na makanjanja tu yaaani wahasibu ambao hawana CPA" kwa mujibu wa Bwana Ludovick Utouh ambae ni mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali -CAG !

Sioni sababu ya NBAA kuendelea kutunga mitihani migumu ya kukomoana wakati Taifa lina upungufu mkubwa sana wa wahasibu wenye sifa za kuitwa wahasibu. Kwa mtazamo wangu mimi kuwatungia watahiniwa mitihani migumu si kwamba
ndio eti utapata wataalamu wa uhakika, si kweli. Kama ingelikuwa ni hivyo mitihani ya inayotungwa na Bodi ya ma-engineer inaongoza kwa kuwa migumu lakini kila siku tunashuhudia maghorofa yakianguka tena yakiwa yanasimamiwa na hao hao ma-engineer wenye sifa.

Mimi sijasikia mitihani ya bodi ya udakitari kwa hapa kwetu Tanzania. Lakini mbona hawa watu wanasoma na baada ya hapo wanalitumikia taifa, bila kupoteza muda mwiiiiiiiiiiiiiiingi wakifanaya mitihani ya bodi yao. Basi kama vipi vyuo vinavyofundisha uhasibu vifungwe na watu wote Tanzania nzima wawe wanafanya hiyo mitihani ya NBAA. Kwa sababu mtu anafaulu vizuri kabisa vyuoni. Kwa mfano kama mimi mwenyewe nina Masters. Lakini mtu huyu huyu akienda kufanya mitihani ya NBAA kila session anaambiwa amefeli. Hivi ni mitihani gani special hiyo inayotolewa na NBAA ambayo vyuo vingine vinashindwa kuitoa ?

Au ndio wapo katika lengo hilo hilo kwamba hawataki watu wengi wawe na CPA. Yaani huu uhaba wa watu wenye CPA wao NBAA wanafaidika nao, kwa kutengeneza mabilioni ya pesa kupitia watahiniwa wao. Halafu mbona wapo watu wenye CPA na tukiwaita kufanya Interview wanashindwa pamoja na CPA zao makwapani. Imefikia mahala Watanzania tumegeuka kuwa na elimu vyeti tu. Yaani unakuta mtu ana vyeti zaidi ya kumi lakini analisaidia nini taifa , hakijulikani !

Tunarudia tena na tena, tunakuomba Mheshimiwa Waziri Mkuu unda tume kuchunguza pale NBAA kuna nini ? Mbona watahiniwa wake wanafeli sana ? KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI !
 
Ni hivi majuzi tu Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda aliunda tume kuchunguza sababu za kufeli kwa wanafunzi wa Form Four iliyopelekea kuwa na matokeo mabaya nchi nzima.

Tunakuomba Mheshimiwa Waziri Mkuu kuunda tume nyingine ili kuchunguza kuwepo kwa matokeo mabovu kila mwaka kwa miaka nenda rudi kwa watahiniwa wa mitihani ya CPA (Certified Public Accountant) inayotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa mahesabu (NBAA).

Tunasema kuna umuhimu wa kuunda tume kuchunguza bodi hii kutokana na ukweli kwamba mitihani inayotolewa na bodi hii ni ya kukomoana sana.Lengo lao ni kuhakikisha kwamba wanaopata hiyo CPA wawe wachache mno. Kwa mfano wanaweza wakafanya mitihani hiyo watahiniwa zaidi ya elfu tatu (3,000) lakini watakaopata hiyo CPA ni chini ya watahiniwa mia tatu tu (300).

Sisi wahasibu tunaona bodi hii haikuundwa kuendeleza taaluma hii ya uhasibu bali ni kuididimiza taaluma hii ili kuwe na wahasibu wachache mno wenye sifa za kuitwa wahasibu. Kwa sababu kwa mujibu wa Ndugu Ludovick Utouh ambae ni mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) anamtambua mhasibu ni yule mwenye CPA tu. Hawa wengine wanaofanya kazi za uhasibu lakini hawana CPA wanajipendekeza tu na ndio wanaoharibu kazi na sifa za taaluma ya uhasibu.

Bodi hii ya NBAA imejihakikishia maisha ya kifahari kwa kila mtumishi wake kutokana na kukusanya mabilioni ya pesa ya bure kutoka kwa watahiniwa wa mitihani yake.

Kwa mfano hii sheria waliyoiweka ya kwamba Mtahiniwa akifanya mitihani na kufaulu somo moja basi wanalifuta, ni sheria kandamizi yenye lengo la kuwarudisha nyuma watu wanaopenda kujiendeleza katika fani hii na vile vile kuleta aina mpya ya UTUMWA kupitia sekta ya elimu. Yaani mtu atumie robo tatu ya umri wake wa kufanya kazi akiwa anasoma.

Sisi binafsi(Wahasibu) hatuelewi kama mtu somo amefaulu eti kwa kuwa ni moja linafutwa kwa nini ? Wakati mpaka huyo mtu amelifaulu hilo somo ametumia rasirimali chungu nzima ikiwemo Muda,Fedha na Jitihada kubwa mpaka kufaulu somo hilo.

Imefikia mahala waajiri wengi hawataki kuwalipia wala kuwaruhusu wafanyakazi wao kufanya mitihani hii kwa kuwa wameona ni kupoteza muda na rasilimali tu. Mtu badala ya kutumia muda wake mwingi katika kufanya kazi ili kuinua uchumi wa taifa, badala yake anatumia muda mwingi kusomea CPA ambayo kuipata kwake ni mpaka Mabwana wakubwa wa NBAA watakapokuwa tayari kukupa. Tunasikitika sana kuona nchi kama ya Uingereza ambayo imetuacha mbali mno kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla, ukifanya mitihani yao ya ACCA hata kama ni somo moja moja na ukafulu wanali-record na unamalizia mengine yaliyobaki. Lakini kwa NBAA ukifaulu somo moja wanalifuta.

Kwa kumalizia tunakuomba Mheshimiwa Waziri mkuu, usisubiri mpaka kutokee maandamano unda tume kuchunguza utendaji kazi wa Bodi ya NBAA kwani imekithiri kwa kufelisha watahiniwa wake kwa makusudi.
click here: Bodi ya wahasibu N.B.A.A mnatutia aibu kimataifa, badilikeni sasa
 
Nadhani mpaka utoe rushwa ndio unapewa cpa. Ukisoma MBA na wenye cpa utashangaa wengi wako kaputi na hawamalizi. Sawa kabisa mkuu, iundwe tume huko kuna urasimu wa ovyo kabisa.
Ushawahi kuona mtu ana fail master's?
 
Back
Top Bottom