Waziri Mkuu wa Ethiopia ataka Jumuiya ya Kimataifa isiingilie mzozo wa Tigray

Waziri Mkuu wa Ethiopia ataka Jumuiya ya Kimataifa isiingilie mzozo wa Tigray

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ameiambia jumuiya ya kimataifa isiingilie mzozo wa jimbo la Tigray, katika kipindi hiki ambacho muda wa mwisho wa masaa 72 aliowapa waasi katika jimbo hilo wajisalimishe ukifikia ukingoni. Katika taarifa yake kiongozi huyo amesema Ethiopia kama taifa huru lina haki zote kusimamia sheria zake na kuzitekeleza ndani ya mipaka yake.

Licha ya kauli yake hiyo lakini, ujumbe wa Umoja wa Afrika unaowajumuisha marais watatu wa zamani unaelekea mjini Addis Ababa katika juhudi za usuluhishi. Hao ni rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, rais wa zamani wa Msumbiji Joachim Chisano, na Kgalema Motlanthe aliyekuwa rais wa mpito wa Afrika Kusini.

Wakati huo huo, Jake Sullivan aliyeteuliwa kuwa mshauri wa masuala ya usalama wa rais mteule wa Marekani Joe Biden, amejiunga na wanaotoa miito ya kuhimiza mazungumzo kuumaliza mzozo huo wa Tigray.
 
Jumuiya ya kimataifa ina haki ya kuingilia pale inapoona maisha ya raia yapo hatarini.
 
Historia inaonyesha hawa TPLF walipigana kishujaa enzi wakiwa waasi waliposhika madaraka ya Ethiopia wakjisahau na walikuwa na angenda ya kujitenga siku moja, wakawa wajeuri mpaka wanakaidi maagizo halali ya SERIKALI kuu, acha wavune walichopanda wenyewe
 
kwa kauli hii, ile tuzo hakustahili kabisa.
 
Back
Top Bottom