Waziri Mkuu wa zamani Hayati Raila Odinga atunukiwa Nishani ya Heshima Kenya (C.G.H)

Waziri Mkuu wa zamani Hayati Raila Odinga atunukiwa Nishani ya Heshima Kenya (C.G.H)

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Waziri Mkuu wa zamani, marehemu Raila Odinga, ametunukiwa Nishani ya Juu Zaidi ya Heshima Nchini Kenya — Chief of the Order of the Golden Heart (C.G.H), heshima ambayo ni ya juu kuliko zote nchini

Tuzo hiyo imetolewa rasmi na Rais William Ruto Oktoba 20, 2025, wakati taifa likiadhimisha Sikukuu ya Mashujaa


Kwa mujibu wa tangazo la gazeti la serikali lililochapishwa tarehe 20 Oktoba 2025, Raila ametambuliwa kwa ujasiri wake wa kipekee, uvumilivu, kujitolea bila kuyumba kwa misingi ya demokrasia na utawala bora, pamoja na mchango wake mkubwa katika kuendeleza umoja wa Afrika na huduma kwa binadamu wote

1761034538670.png

Akihutubia wananchi katika Uwanja wa Ithookwe, Kaunti ya Kitui, Rais Ruto alimtambua Raila kwa mchango wake mkubwa katika ujenzi wa taifa na urithi wake wa kudumu

Kiongozi wa taifa pia alimtaja Raila kama mzalendo shupavu na shujaa wa vizazi vyote, akisisitiza kuwa maadili aliyoyaishi yanapaswa kuwa mwongozo kwa taifa zima

Heshima hiyo imetolewa siku moja tu baada ya mazishi ya Waziri Mkuu huyo wa zamani katika eneo la Kang’o Ka Jaramogi, Bondo, Kaunti ya Siaya

Raila alifariki dunia tarehe 15 Oktoba 2025, akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Devamatha, Kerala, nchini India

Mwili wake ulirejeshwa nchini Kenya siku ya Alhamisi, Oktoba 16, na akazikwa kwa heshima zote za kitaifa, kama shujaa na kiongozi mashuhuri wa historia ya Kenya

Source: Citizen Kenya
 
Back
Top Bottom