The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema wafanyakazi wanafurahishwa na maboresho wanayofanyiwa na Serikali ya awamu ya sita.
Ameyasema hayo leo Alhamisi Mei 1, 2025 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi’ mkoani yanayofanyikia kitaifa mkoani Singida ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Sherehe hiyo ina kauli mbiu isemayo “Uchaguzi Mkuu 2025 utuletee viongozi wanaojali haki na masilahi ya wafanyakazi sote tushiriki,” ikiwa ni ujumbe unaosisitiza kushiriki uchaguzi mkuu huo.
“Jana wakati nakagua maandalizi ya Mei Mosi nilitembelea ofisi za Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ofisi ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) Mkoa wa Singida.
“Nikapata nafasi ya kuzungumza na viongozi na baadhi ya wafanyakazi kwa pamoja wakanipa salamu zako wakasema wanafarijika na maboresho unayowafanyia wafanyakazi hapa nchini na hawana deni wanalokudai ila wewe unawadai muda ukifika watakulipa,” amesema.
Amesema juhudi za Rais Samia kuboresha mazingira ya kazi, kuongeza fursa za ajira na mazungumzo kati ya Serikali, waajiri na vyama vya wafanyakazi zinanufaisha wafanyakazi nchini.