Waziri Mkuu wanachuo wa Chuo cha Ualimu Northern Moshi wametapeliwa. Wasaidie

Fred Mwakitundu

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
227
Reaction score
382
Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunaamini unaendelea vizuri na mikutano ya uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi kwa chama cha mapinduzi (CCM)hapa mkoani Kilimanjaro na leo upo wilaya ya Rombo kumnadi Profesa Mkenda ambaye tunaamini atapata ushindi wa kishindo.

Mheshimiwa Waziri Mkuu,wakati unaendelea na mikutano ya kampeni katika mkoa wa Kilimanjaro,kuna jambo moja naomba ujaribu kuingilia kati nalo ni hili la watoto wetu waliokuwa wanachukua kozi ya English Medium kwenye chuo cha ualimu cha NorthenHighlands cha mjini Moshi kutapeliwa fedha zao kwa kusoma kozi ambayo haijasalijiwa wa NACTE.

Katika mwaka wa masomo 2018/2019 chuo kiliwadahili wanafunzi zaidi ya 50 kwa kozi hiyo ya miaka miwili na kila mmoja akalipa zaidi ya sh, Milioni tatu kama ada lakini watoto hawa wakanyimwa fursa ya kufanya mtihani wa mwisho juni 29 mwaka huu baada ya kuelezwa hawana sifa za kufanya mtihani baada ya kufukuzwa chuoni hapo.

Swali la msingi kabisa ni kwa nini chuo kikawapokea wanafunzi wasiokuwa na sifa na kuwadahili na kisha kuchukua pesa zao wakati hawana sifa kama siyo utapeli ni nini?

Cha ajabu baada ya kuwafukuza hawa watoto chuo kikatoa vyeti vya kushiriki na kutoa matokeo ya ufaulu,hapa napo kuna shida kubwa,hatujawahi kuona mwanafunzi wa chuo chochote ama wa kozi yoyote kuanzia ngazi ya cheti anapewa cheti cha mahudhurio,hii siyo semina wala warsha ambako waandaaji hutoa vyeti vya ushiriki,huu ni utapeli kama utapeli mwingine.

Mheshimiwa Waziri Mkuu,tunaamini ujumbe huu utaupata kabla hujamaliza ziara yako ya kichama katika mkoa wetu na tunaamini utaufanyia kazi ili kukomesha huu utapeli kwa chuo hiki na vyuo vingine vya aina hii.

Tunakutakia ziara njema hapa Kilimanjaro.
 
Hicho chuo ni kweli kina uhuni Fulani hivi wanawafanyia wanafunzi wanaosoma hapo na lazima kiangaliwe Mara ya pili.

Kwa idara ya sekondari kuna matatizo yamejificha pia, hao wamiliki sijui tatizo nini.
 
Mheshimiwa Waziri Mkuu, tunaamini unaendelea vizuri na mikutano ya uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi kwa chama cha mapinduzi (CCM)hapa mkoani Kilimanjaro na leo upo wilaya ya Rombo kumnadi Profesa Mkenda ambaye tunaamini atapata ushindi wa kishindo.

Mheshimiwa Waziri Mkuu,wakati unaendelea na mikutano ya kampeni katika mkoa wa Kilimanjaro,kuna jambo moja naomba ujaribu kuingilia kati nalo ni hili la watoto wetu waliokuwa wanachukua kozi ya English Medium kwenye chuo cha ualimu cha NorthenHighlands cha mjini Moshi kutapeliwa fedha zao kwa kusoma kozi ambayo haijasalijiwa wa NACTE.

Katika mwaka wa masomo 2018/2019 chuo kiliwadahili wanafunzi zaidi ya 50 kwa kozi hiyo ya miaka miwili na kila mmoja akalipa zaidi ya sh, Milioni tatu kama ada lakini watoto hawa wakanyimwa fursa ya kufanya mtihani wa mwisho juni 29 mwaka huu baada ya kuelezwa hawana sifa za kufanya mtihani baada ya kufukuzwa chuoni hapo.

Swali la msingi kabisa ni kwa nini chuo kikawapokea wanafunzi wasiokuwa na sifa na kuwadahili na kisha kuchukua pesa zao wakati hawana sifa kama siyo utapeli ni nini?

Cha ajabu baada ya kuwafukuza hawa watoto chuo kikatoa vyeti vya kushiriki na kutoa matokeo ya ufaulu,hapa napo kuna shida kubwa,hatujawahi kuona mwanafunzi wa chuo chochote ama wa kozi yoyote kuanzia ngazi ya cheti anapewa cheti cha mahudhurio,hii siyo semina wala warsha ambako waandaaji hutoa vyeti vya ushiriki,huu ni utapeli kama utapeli mwingine.

Mheshimiwa Waziri Mkuu,tunaamini ujumbe huu utaupata kabla hujamaliza ziara yako ya kichama katika mkoa wetu na tunaamini utaufanyia kazi ili kukomesha huu utapeli kwa chuo hiki na vyuo vingine vya aina hii.

Tunakutakia ziara njema hapa Kilimanjaro.
Hawa watotot wasaidiwe. Vyuo vya binafsi vinafanya hivyo.
 
Inawezakanaje mwanafunzi unamsajili,unachukua ada yake zaidi ya milioni tatu,anasoma miaka miwili,inafika muda wa kufanya mtihani wa mwisho unamwambia hana sifa unamfukuza chuoni.hii imekaaje jamani?.

Cha kushangaza zaidi,wanafunzi unampa cheti cha mahudhulio(Certificate of Attendance) na hapo hapo cheti hicho kimeandikwa chini yake "Has Successfully completed Education Training Programme for English Medium Primary Schools from 2018 to 2020 with a good perfomance" na alama akawekewa hapo chini.

Huyo ni mwanafunzi anayeambiwa hana sifa,sasa lini alifanya mtihani na hizo maksi akazipataje?

Tunahitaji mjadala mpana kuhusu huu utapeli vinginevyo watoto wetu wataendelea kulizwa sana
 
Vijana wasaidiwe.... Kupotezeana tu muda, mtoto anasoma wee unakuja kumpa cheti cha mahudhurio
 
Takukuru Kilimanjaro fanyeni kazi hiyo mezani au mnasubiri mpaka ziara ya Magufuli aje atatue na hili tatizo.Mkuu wa Mkoa na Wilaya na watu wa TISS wote mpo humu tumsaidie Magu na Waziri Mkuu kazi ndio hizi sasa.

Cc Mh Mbunge wa Rombo
 
Back
Top Bottom