Tatizo umeleta uzi kimahaba mahaba hujakaa utulie uelewe taarifa ili uandike vizuri kitu cha kueleweka.
Umesema waziri ilhali picha iliyobandikwa na Mkenya inasema gavana, pili sio kwamba ikibandikwa na Mkenya basi ndio inapata uhalali, maana haijaja kupitia kituo maalum cha habari, mtu kabandika tu mapicha ambayo hayaonekani kuendana.
Kingine, fahamu kwetu mawaziri hawajihusishi na mambo madogo madogo ya ovyoo, sio kama kwenu nchi ya ajabu ajabu waziri mzima mwenye dhamana ya uwaziri nchi yote, anayeitwa Lugola bila aibu anamtetea Gwajima kuhusu mambo ya kipumbavu ambayo wenyewe tuliona video kabisa.
Kuna kipindi nilishangaa waziri Mwakyembe anaingilia bifu la wasanii, anaagiza Dudu Baya atiwe ndani kisa amemkosoa marehemu Ruge, upumbavu sana kwa waziri ambaye anategemewa kujishughulisha na mambo muhimu ya kuendeleza nchi anapoteza muda wake kukimbizana na wasanii huku akiwafunga jela.
Hayo tu ni matukio machache, kuna mengine mengi ya ovyoo nikiandika humu nitajaza server za watu bure.