Waziri Mpango umenena kuhusu Mamlaka ya Mapato Tanzania

dndagula

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
1,602
Reaction score
1,650
Nimemsikiliza Waziri Mpango wakati akiongea na maafisa wa TRA nchini kuhusu kukusanya kodi na kufikia lengo la tr.2.

Nimependa na kuafiki kwa vile miradi mingi itakamilika kwa fedha ya ndani. Kitu ambacho amewaasa maafisa hao wazingatie ni kukusanya kodi kwa weledi, uaminifu na kwa hekima na busara ili kuifanya sekta binafsi kushamiri na ukusanyaji kodi kuwa endelevu.

Waziri alionya kuhusu kubambika kodi na kisha kuomba rushwa. Mimi ninakubaliana na waziri iwapo TRA hawatakuwa na njia rafiki za kukusanya kodi na kuwa wabunifu hawatafikia malengo hayo.

Rais aliwahi kuwaambia wapanue wigo wa kodi itozwe kwa watu wengi hata kama ni kidogo kidogo lakini kwa kupanua mzunguko wa ukusanyaji wake. (Kodi ya Tanzania inabebwa na idadi kubwa ya watu m. 56.)

Aidha wanapaswa kubadili mtizamo wao kwa wafanyabiashara wawachukulie kama washirika kibiashara na hivyo mitizamo ya kukomoa iachwe.

Pia kitengo cha elimu kitumike mno kuelemisha wafanya biashara na wananchi kwa ujumla badala ya kuvizia wafanye makosa na kisha kuwapiga faini zisizolipika. Hili litaua sekta ya biashara na kuikosesha serikali mapato endelevu. Mifumo ya teknolojia na elektroniki itumike zaidi katika ukusanyaji kodi.

Kuhusu tozo zipunguzwe viwango na idadi ili zilipike. Na hili lifanyike mapema mno. Itasaidia. Utaratibu wa sasa kutegemea faini na riba tu ni wa mpito si endelevu na itafika mahala utashindikana kwa vile wafanyabiashara watashindwa kulipa na kufunga biashara zao kwa vile ni makadirio nje ya faida- ni adhabu- na muda mwingi kuutumia mahakamani kwenye mashauri ya kodi.

Pamoja na wito na maelekezo ya waziri Kufikia malengo yasitafisriwe na maafisa wa TRA kama ni mapambano na kukomoa. Kamishna Mkuu ndg Mhede awe makini kwa kuwasimamia watendaji kwa karibu ili kufikia malengo bila kusababisha maumivu kwa wananchi na kuathiri biashara zao na hapo hapo kuchukua hatua kwa wala rushwa bila kuonea.
 
‘Rais aliwahi kuwaambia wapanue wigo wa kodi itozwe kwa watu wengi hata kama ni kidogo kidogo lakini kwa kupanua mzunguko wa ukusanyaji wake.’

Teh teh teh na wewe ukaamini kweli anamaanisha?
Mimi niliamini hivyo kwa vile maelekezo hayo ya Rais yana dhima ya kisera. Ni suala la wao kutekeleza tu.
 
Kuna wale maofisa vinara wa kuwabambikia kodi kubwa wafanyabiashara kuwafungia Account zao kienyeji kwa njia haramu za kishetani watachukuliwa hatua gani?
 
Uongozi wa TRA kwa kushirikiana na MoF wanapaswa kuwa wabunifu na kuja na mikakati mipya na ya kisasa ktk kupanua wigo wa kodi na kutafuta nyanzo vipya vya mapato. Njia zinazotumika kwa sasa kwa mazoea zimejikita ktk vyanzo vile vile ambavyo vimezoeleka.

Sehemu kubwa ya kodi hukusanywa kutoka ktk sekta iliyokuwa rasmi ambayo ni rahisi sana kuifikia kwa njia za mazoea. Sekta hii hufahamika vyema mbele ya macho ya wenye mamlaka ya kukusanya kodi, kwa hiyo walipa kodi waliopo ndani ya sekta hii hawana namna yoyote ile ya kuweza kukwepa kuonekana kwa mapato yao yaliyopo ktk shughuli zao za kila siku.

Jicho la TRA linapaswa kujikita katika kila shughuli zenye kuwaingizia watu vipato iwe ndani ya sekta rasmi hata pia ile isiyokuwa rasmi. Ni lazima wajibu wa kulipa kodi umfikie kila raia raia ambaye ni mwenye "taxable income". Hapa ndipo tunapoona ukweli kuwa TRA imeshindwa kwa kiasi kikubwa kukusanya kodi ktk sekta isiyo rasmi ikiwa kama sehemu muhimu ya kupanua wigo wa kodi hapa nchini.

TRA inapaswa kuwa na kitengo mathubuti cha utafiti wa kodi ili kutambua kodi nyingi zilizojificha ktk sekta isiyokuwa rasmi. Aidha inapaswa kuwa kitengo cha intelejensia ambacho kazi yake maalum itakuwa ni kuiangalia sekta hii sambamba na sekta iliyokuwa rasmi endapo kuna "tax potentials" zilizopo kutokana mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Vilevile mamlaka inaweza kuangalia uwezekano wa kukusanya kodi kutoka ktk sekta hii kwa njia ya ukusanyaji wa kodi kwa uwakala kupitia kampuni binafsi ambazo zitapewa utaratibu ambao unaweza kufanikisha "monitoring and collection of taxable income within informal sector"
 
‘Rais aliwahi kuwaambia wapanue wigo wa kodi itozwe kwa watu wengi hata kama ni kidogo kidogo lakini kwa kupanua mzunguko wa ukusanyaji wake.’

Teh teh teh na wewe ukaamini kweli anamaanisha?
Kwa hiyo unadhani alipotoka pale aliwaambia hao watendaji kuwa alikuwa anazuga tu au ni kazi ya wakusanyaji sasa kutumia uwezo wao kupanuwa wigo huo bila kuathili biashara hizo?
 
Binafsi naamini ikiwa TRA watatoa elimu ya kutosha kupitua redio, television, matangazi ya wasanii kama kina Joti, Diomond nk, watajikuta wanafikia hicho kiwango mapema sana. Ninachoona mimi wananchi hawana elimu ya kutosha ya mlipa kodi.

Nashauri pia hii elimu ya mlipa kodi ianza kufundishwa mashuleni kuanzia msingi hadi chuo, hii itasaidia sana hata watoto wakienda nunua kitu dukani nao watadai risití na hata wakija kuwa wafanya biasgara huko mbeleni wataelewa nini maana ya kulipa kodi.
 
Kwa hiyo unadhani alipotoka pale aliwaambia hao watendaji kuwa alikuwa anazuga tu au ni kazi ya wakusanyaji sasa kutumia uwezo wao kupanuwa wigo huo bila kuathili biashara hizo?

Yaani mtu anakunyima mkono wa salamu na bado unamsainia malipo ya yeye kwenda kutibiwa nje?hiiiiiiiii ingekua ni mimi wafaaaa.
 
Mimi niliamini hivyo kwa vile maelekezo hayo ya Rais yana dhima ya kisera. Ni suala la wao kutekeleza tu.
Rubbish! Unaamini maneno yasiotekelezwa?! Haya maneno yamekuwepo sana long time.
Anyways kwa upande mwingine labda useme na mi naami hivo kwamba yakitekelezwa ni mawazo mazuri.
 
Wawekezaji wapya ambao wapo kwenye trends ya uwekezaji waruhusiwe haraka sana na wapewe kila aina ya msaada
Ucheleweshwaji wa mizigo bandarini umalizwe kabisa iwe siku tatu mtu atoe nzigo wake
Paypal ianzishwe haraka sana hapa pana fedha nyingi mno maana watu watakuwa free kuagiza mizigo yao na wakati inakuja nchini serekali itapata chochote kingi mno sama e money gain
Tuanze kutoa citizen ship kwa watu wanaoitaji kuwekeza tanzania wenye mitaji ya dollar 500000$ money should be deposited to bot
Bila kubuni plan zingine mpya wananchi wataumia sana shida ni kwamba TRA wanapoambiwa zidisheni mapato wao wanatupia jicho kwa huyu mtanzania ambaye yupo hoi jinsi ya kufirimba badala ya kupanga au kutengeneza njia zingine mpya
 
Kuna ubaya gani tukafungua baadhi ya njia ambazo tumezifunga za kimapato mfano kilimo cha mirungi na kusafirisha nje
mfano morroco ni taifa tajiri kwa namna fulani ambalo limewahi kutusaidia, tegemeo lake kubwa ni UTALII,na kingine ni hiki ambacho kinaingiza mapato kwa fujo #ARDHI KUBWA NZURI TUNAYO HAKUNA KISINGIZIO HAPA
###############
Fact: According to a study from 2019, around 70% of the cannabis consumed in Europe comes from Morocco.
 
Naomba nishauri maeneo yafuatayo yafanyiwe kazi ili kongeza wigo wa kulipa kodi. Tanzania imebahatika kuwa ns idadi kubwa ya watu na raslimali nyingi zitumike kuongeza kodi.Hatua zifuatazo zichukuliwe haraka sana kuongeza wigo:
1. Kutoza kodi ya moja kwa moja( Direct Tax) kwa watu wote 18 years wenye kipato ili kuchangia mfuko maalum wa Maendeleo ninaoupendekeza kuanzishwa kwa miradi ya SGR, Bwawa la Umeme na Daraja la Busisi-Kigongo nje ya kodi inayotozwa inaweza kuitwa kodi au tozo. Hii itatoa uhakika wa kuikamilisha kwa muda na kasi. Kodi au tozo hii ifanane na kodi ya kichwa ingawaje hii itakuwa tofauti na itegemee pato la mtu km ifuatavyo:
a. Biashara kubwa walio kwenye VAT walipe shs 50000 kwa mwezi
b. Biashara za kati(middle income business)kipato cha m20 -100 kodi shs 20000 kwa mwezi
c. Wafanyabiashara wadogo( machinga, bodaboda, ntilie, nk) shs 2000 kwa mwezi
d. Taxi rasmi shs 5000 na taxi bubu zisizoandkishwa zirasimishwe zilipe 10000 kwa mwezi
e. Wafugaji kuku, ngombe nk mijini 10000 kwa mwezi
f. Kilimo cha kati Bustani na mbogamboga mijini shs 10000 kwa mwezi
g. Kilimo kijijini 2000 kwa mwezi na wafugaji kijijini shs 200 kila mfugo kwa mwezi
h. Wavuvi shs 10000kwa mwezi
I. Wachimbaji wadogo madini shs 10000 kwa mwezi
J. Mafundi binafsi i.e washi, mchundo, umeme, makenika etc ambao ni wajasiria mali mijini 3000 na vijijini 2000 kwa mwezi
k. Kazi na biashara nyinginezo wasusi, vinyozi, waganga wa kienyeji, waigizaji, muziki, matumizi ya teknolojia i.e TV na yeyote mwenye pato halali alipe 5000 kwa mwezi.(wasiokuwa na biashara au shughuli zisizotambulika rasmi ie malaya wanaojiuza nao wawekewe utaratibu)

Tiketi za wasafiri kwenye vituo vikuu vya mabasi nazo zilipiwe asilimia 1 kwa kila msafiri km ilivyo kwenye viwanja vya ndege

Sasa fikiria fedha kiasi gani itapatikana kwenye mfuko huo kukamilisha miradi hiyo haraka bila misaada nje ya nchi. Changamoto za msingi ni menejimenti ya makusanyo yenyewe yatakayo hitaji njia na mbinu mbalimbali mfano
1.kuongeza idadi ya maafisa wa TRA na kuanzisha vituo vidogo vya kata au kushirikiana na maafisa kata au serikali za mitaa
2.kutembelea maeneo ya ukusanyaji
3 kutumia teknolojia ya kieletroniki na mitandao hasa simu
4. Elimu itolewe kwa njia mbalimbali
5.idara ya utafiti ya TRA na compliance iimarishwe.Kwa kufanya hivi mtakwepa kuegemea njia zilizooeleka kukusanya kodi(traditional sources of taxation) nothing is not taxable income mkitaka kuongeza mapato ila informal sector ni kubwa na haitozwi kodi badilikeni.

B.Kukata kodi posho za wafanyakazi
Kuna haja ya kuangalia uwezekano wa kukata tozo au kodi kwa posho zote zinazolipwa na serikali kwa watumishi wake au sekta binafsi kwa wafanyakazi wake asilimia 1 kwa kila malipo
C.kupunguza misamaha ya kodi
Ni wakati pia wa kuangalia namna nzuri ya kuondoa misamaha ya kodi kwa makanisa na misikiti na mashirika ya dini isipokuwa kwa vitabu vitakatifu tu. Aidha zitozwe pesa ya ushuru kidogo sana kuondoa malalamiko ili nao wachangie kwenye kodi.wakae nao kujadili
D.Kodi ya utaalamu na ujuzi na ubingwa(intellectual property tax)
Kuna haja ya kutoza kodi za utaalam, na uvumbuzi utakaolipiwa kodi na kisha kuandikishwa na kutambuliwa kitaifa
 
Naomba nishauri maeneo yafuatayo yafanyiwe kazi ili kongeza wigo wa kulipa kodi. Tanzania imebahatika kuwa ns idadi kubwa ya watu na raslimali nyingi zitumike kuongeza kodi.Hatua zifuatazo zichukuliwe haraka sana kuongeza wigo:
1. Kutoza kodi ya moja kwa moja( Direct Tax) kwa watu wote 18 years wenye kipato ili kuchangia mfuko maalum wa Maendeleo unaopendekezwa kuanzishwa kwa miradi ya SGR, Bwawa la Umeme na Daraja la Busisi-Kigongo. Hii itatoa uhakika wa kuikamilisha kwa muda na kasi. Kodi au tozo hii ifanane na kodi ya kichwa ingawaje hii itegemee pato la mtu km ifuatavyo:
a. Biashara kubwa walio kwenye VAT walipe shs 50000 kwa mwezi
b. Biashara za kati(middle income business)kipato cha m20 -100 kodi shs 20000 kwa mwezi
c. Wafanyabiashara wadogo( machinga, bodaboda, ntilie, nk) shs 2000 kwa mwezi
d. Taxi rasmi shs 5000 na taxi bubu zisizoandkishwa zirasimishwe zilipe 10000 kwa mwezi
e. Wafugaji kuku, ngombe nk mijini 10000 kwa mwezi
f. Kilimo cha kati Bustani na mbogamboga mijini shs 10000 kwa mwezi
g. Kilimo kijijini 2000 kwa mwezi na wafugaji kijijini shs 200 kila mfugo kwa mwezi
h. Wavuvi shs 10000kwa mwezi
I. Wachimbaji wadogo madini shs 10000 kwa mwezi
J. Mafundi binafsi i.e washi, mchundo, umeme, makenika etc ambao ni wajasiria mali mijini 2000 kwa mwezi
k. Kazi na biashara nyinginezo wasusi, vinyozi, waganga wa kienyeji, waigizaji, muziki, matumizi ya teknolojia i.e TV na yeyote mwenye pato halali alipe 5000 kwa mwezi.

Tiketi za wasafiri kwenye vituo vikuu vya mabasi nazo zilipiwe asilimia 1 kwa kila msafiri.

Sasa fikiria fedha kiasi gani itapatikana kwenye mfuko huo kukamilisha miradi hiyo haraka bila misaada nje ya nchi. Changamoto za msingi ni menejimenti ya makusanyo yenyewe yatakayo hitaji njia na mbinu mbalimbali mfano
1.kuongeza idadi ya maafisa wa TRA na kuanzisha vituo vidogo vya kata au kushirikiana na maafisa kata au serikali za mitaa
2.kutembelea maeneo ya ukusanyaji
3 kutumia teknolojia ya kieletroniki na mitandao hasa simu
4. Elimu itolewe kwa njia mbalimbali
5.idara ya utafiti ya TRA na compliance iimarishwe.Kwa kufanya hivi mtakwepa kuegemea njia zilizooeleka kukusanya kodi(traditional sources of taxation) nothing is not taxable income mkitaka kuongeza mapato ila informal sector ni kubwa na haitozwi kodi badilikeni

B.Kukata kodi posho za wafanyakazi
Kuna haja ya kuangalia uwezekano wa kukata tozo au kodi kwa posho zote zinazolipwa na serikali kwa watumishi wake au sekta binafsi kwa wafanyakazi wake asilimia 1 kwa kila malipo
C.kupunguza misamaha ya kodi
Ni wakati pia wa kuangalia namna nzuri ya kuondoa misamaha ya kodi kwa makanisa na misikiti na mashirika ya dini isipokuwa kwa vitabu vitakatifu tu. Aidha zitozwe pesa ya ushuru kidogo sana kuondoa malalamiko ili nao wachangie kwenye kodi.wakae nao kujadili
D.Kodi ya utaalamu na ujuzi na ubingwa(intellectual property tax)
Kuna haja ya kutoza kodi za utaalam, na uvumbuzi utakaolipiwa kodi na kisha kuandikishwa na kutambuliwa kitaifa.
Pengine maeneo yenye utata na chamgamoto kutozwa kodi au tozo ni yale "covert" yasiyotambuliwa na serikali kisheria mf malaya, wauza gongo, madalali bubu nk hapa sheria ya kodi na kanuni ziangaliwe upya.
KUIPITIA SHERIA
Ili kuongeza wigo hapa sheria lazima ipitiwe kuingiza mabadiliko na hususani kuifanya kodi iwe realistic mf maeneo ya faini kubwa ni vikwazo mno. Hazilipiki na huzalisha rushwa bila sababu.
 
JF ina nguvu kubwa sana ! bila JF kufumua uozo sidhani kama Mpango angejitokeza .

Mungu ibariki JF
 
TRA njooni kwenye huu uzi mtapata njia nzuri za kuboresha makusanyo bila kutumia nguvu nyingi
 
Mkuu,
unaitamka elfu 10 Kama pesa ya mchezo mchezo Kwa watu wa kipato Cha chini.

Uku mtaani watu wanashindwa mpaka kulipa Kodi ya chumba Cha kulala Cha elfu 5 kwa mwezi.

Afu uyo uyo alipe Kodi ya elfu 10 serikalini?

HEBU TOKA UKO DASLAM,
UENDE MIKOANI UONE MAISHA JINSI YALIVO MAGUMU
 
Nimemsikiliza Waziri Mpango wakati akiongea na maafisa wa TRA nchini kuhusu kukusanya kodi na kufikia lengo la tr.2.

Nimependa na kuafiki kwa vile miradi mingi itakamilika kwa fedha ya ndani.

Uchumi una realities zake. Hauendeshwi kwa maazimio. Hili lengo la kukamilisha miradi kwa “fedha za ndani” limezingatia uhalisia? Kuna ulazima wa kufanya hivyo hata kwa maumivu makubwa kwa wananchi?

Na dhana ya “fedha za ndani” inayopigiwa chepuo na serikali ni kitu gani hasa? Inaeleweka? Mara kadhaa tumeambiwa kuwa Hata mikopo ni fedha za ndani kwa vile serikali/kodi zetu zitalipa!

Isije ikawa ni namna nyingine ya kutwisha wananchi mzigo wasio na kauli nao. Inaweza pia kuwa fursa mpya ya kifisadi kwa vile hizo pesa haziathiriwi na “masharti ya donors” na ripoti zake huishia mamlaka za ndani wakati mwingine bila hata CAG kuhusika.
 
Hakuna maendeleo yasiyokuwa na maumivu muhimu kodi ikusanywe kimkakati na matumizi yake yende kunakopaswa.
 
Kuna wale maofisa vinara wa kuwabambikia kodi kubwa wafanyabiashara kuwafungia Account zao kienyeji kwa njia haramu za kishetani watachukuliwa hatua gani?

Wafanyabiashara sasa muda umefika wa kuanza kuwa wakweli. Hawana msaada wowote. Wanachokwambia wanafanya leo, Kesho hao hao TRA wanakirudisha tena mizani, na fain juu. Rushwa inayoendelea kwenye mamlaka hii, sababu ya mwanya wa kutoa assessment kubwa ni balaa.
Nataka kujua mtu anapokuja anadai mil 100,halafu kienyeji enyeji inarudi mil 20, nao wanaangaliwaje? Otherwise ntaamini hawa maafisa wana Baraka za wanaowatuma
 
Back
Top Bottom