Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Mmojawapo wa mawaziri wa Kenya aitwaye Kipchumba Murkomen ameomba msamaha kutokana na mtindo wake wa maisha ya ufahari aliokuwa akiishi ambao ulikuwa ukiwakwaza Wakenya wengi.
Baada tu ya kupata uwaziri huyu bwana alikuwa akivaa nguo, viatu na saa za anasa ambavyo ni designer brands kutoka nchi za Ulaya na Marekani pamoja na hayo alikuwa akienda Manchester United mara kwa mara kuangalia mechi za timu yake pendwa Man U inapocheza na timu kubwa.
Wakenya wengi walikuwa wakilalamika na kupiga sana kelele aina hiyo ya mtindo wake wa maisha wakihoji waziri ambaye haieleweki anafanya biashara gani nje ya uwaziri amepata wapi pesa nyingi hivyo za kuishi maisha ya anasa mbele ya maisha ya umma.
Hatimaye baada ya kutumbuliwa katika kibarua chake cha waziri wa miundombinu hivi karibuni kufuatia maandamano makubwa ya Gen Z ameibuka na kudai amefanya tafakari kubwa ya mtindo wake wa zamani wa maisha na anaomba msamaha kwa wote aliowakwaza!