Waziri mpya wa Mawasiliano, anza kazi na Azam Media. Wamepanga kutupiga kwenye vifurushi vipya

Waziri mpya wa Mawasiliano, anza kazi na Azam Media. Wamepanga kutupiga kwenye vifurushi vipya

Kwani Azam wanapata ruzuku serikalini? Hii ni biashara ya mtu binafsi na mfanya biashara yoyote lengo ni faida. Haya mambo hayamuhusu waziri wala serikali ni maamuzi ya kampuni binafsi hata sokoni tunaenda tunakutana na bei mpya lakini tunanunua. Kwa Azam kama huliwezi ni kuhamia sehemu unayoweza hakuna aliyelazimishwa kununua.
Upo sahihi kabisa japokuwa starehe ni gharama ila wanatoza gharama kubwa Sana
 
Azam wameleta VAR sasa wamepanga kutupandishia vifurushi vya ving'amuzi!

Hii si sawa bora wapate mpinzanj kwenye kuonesha ligi za nyumbani ili wasitunyanyase!
Biashara huru, kwani walikulazimisha kutumia huduma zao?

VAR inatumiwa na wasimamizi wa soka kiwanjani, siyo shirika la utangazaji. kama AZAM wameleta basi wanaoitumia wataikodisha.
 
Kwa hapa ndani ana competitors kama dstv , startimes , zuku n.k .zaidi ya dstv hakuna service provider mwengine hapo anaeweza kuwa programs alizonazo azam mshindani mkuu wake ni dstv ambaye watanzania wengi wameshindwa afford service unataka watu waende wapi?
Umeandika kiswahili lakini nimepata ugumu kuelewa
So Bei ya Azam ipo chini kulinganisha na zuku? Startimes? Au kulinganisha na dstv?
 
Hivi nchi za wenzetu,ivi vitu ni gharama namna hii?? Vp na internet bundle??sema levels za maisha kwa apa bongo ni tofauti ukiwaza ulipe kodi ya nyumba,ulipie bills za umeme+maji,na vifurushi vya king'amuzi navyo kulipia😂😂
Anaepata leseni ya kuonesha ligi ya ndani awe anapewa bei elekezi siyo kupandisha vifurushi kiholela kisa hatuna option
 
Ndugu Mteja, kuanzia 1/8/24 kutakuwa na mabadiliko ya bei. Kifurushi cha 25000 kuwa 28000; 17000 kuwa 19000; 10000 kuwa 12000; 6000 kuwa 7000 na 3000 kuwa 4000.

Azam decoder hawana Ubora kuzidi Dstv, Wanatumia kigezo cha kutuonyesha mipira Ili kuchaji gharama zaidi, ongezeko hilo ni kama blackmailing, hakuna media nyingine wanaowapa ushindani kwenye mpira kwa Sasa. Ongezeko hilo sio halisia na maisha ya wananchi, ajabu Mzawa mwenzetu anatunyonya kuliko wageni wawekezaji.

Mmesubiri home boy apigwe chini ndio mlete ongezeko! Waziri nakusihi, liangalie kwa jicho la wananchi wanyonge..


Amia zuku au star times
 
UMEPEWA WIZARA HII ILA KUNA DUDE HILI LINAWATAPELI WATANZANIA KILA KWENYE MASHINDANO MAKUBWA YA KIDUNIA

1.Mwaka juzi walituhadaa tulipie vifurushi vyote wataonesha kombe la dunia lilipigwa kule France , hawakufanya hivyo tukabaki kulalamika bila majibu hadi mashindano yale yakaisha , utapeli

2.Mwaka huu kwenye Euro wametupiga tena unajua kuna match unakuta kuna mawaidha ya masheikh,au ni mbunu ya kutulazimisha kusikiliza uislamu wao .


3.Sasa ni Olympic wanatangaza kila saa na channel hizi ni zile za kulipia , tunanunua vifurushi lakini hakuna kitu

OMBI ,Kama ulivyokuwa unapitia kwenye wezi wa viwanja hebu pitia kwa hawa jamaa , tumechoka na utapeli huu


USSR
 
Uko sahihi kabisa,hawa jamaa ni matapeli wanaoiba huku wanatabasamu......
 
Kama utaki longolongo kwenye mashindano yoyote ya michezo ya kimataifa ni heri kutumia DSTV,hao Azam bado wachanga sana kwenye hizo mambo ndo maana maneno mengi halafu utekelezaji wa ovyo.
 
Back
Top Bottom