Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuweka bei elekezi katika huduma na bidhaa inazonunua
"Kwanini nchi nyingine za jirani na mashirika ya kimaitaifa wananunua magari kwa bei nafuu pengine zaidi ya nusu kuliko sisi serikalini" alihoji Nchemba
"Haiwezekani hata kidogo lazima tukomeshe hali hii na tunaitegemea zaidi PPRA kutusaidia kutukwamua kutoka hapa ndani ya kipindi cha miezi michache katika mwaka huu wa fedha"alisema Mwigulu
Chanzo: Gazeti la Mwananchi Julai 15, 2022
Walianze hili haraka sana.Utekelezaji ndio shughuli nzito kwelikweli.
Utaratibu wa tenda unasababisha mtu anayetenda,kuingia gharama za ziada tofauti na utaratibu wa quatation. Hata iweje kama kitu kitanunuliwa kwa tenda bei yake itakuwa juu tu. Mfano yale makabrasha ya tenda wazabuni wanauziwa hiyo tayari ni gharama. Pili lazima walete dhamana ya benki nayo pia ni gharama tatu kuna document ya mwanasheria lazima waambatanishe hiyo nayo ni gharama, pia wanatakiwa wasupply kwanza bure ndipo baadae walipwe hivyo kama .mzigo ni wa mabilioni lazima wakope benki kwa kuchukua overdraft na baadae wakilipa wanalipa kwa riba. Pia mzabuni akishinda inabidi waingie mkataba hiyo mikataba nayo ni gharama. Hayo yote na mengine yanafanya bei ya kitu kinachonuuliwa kiwe juu kuliko ile bei unayoiona imebandikwa dukani. Nakubali kuwa bei elekezi ni muhimu lakini lazime izingatie gharama za ziada ambazo mzabuni anaingia vinginevyo litatengenezwa tatizo lingine la kununua vitu sub standard. Best way ni kununua moja kwa moja kiwandani kama vitu wanavyonunua ni vingi lakini sheria ya manunuzi inakataza kutokana na kipengele cha ushindani ambacbo kinasisitiza watu wasbindane.HAISEE KUMBE HAKUKUA NA LEDGER YA BEI ELEKEZI HUU NI UZEMBE WA HALI YA JUU,NI LAZIMA SEREKALI IWE NA LEDGER YA BIDHAA ZOTE INAZOZINUNUA MARA KWA MARA,KUEPUKA WAPIGAJI, AMBAO HUONGEZA BEI KWA KARIBU MARA MBILI AU TATU, HIVYO KUOKOA PENGINE FEDHA AMBAZO ZINGETUMIKA KATIKA SHUGHULI ZINGINE NYETI.
Ina maana miaka yote upigaji Kama kazi !! Duh ! Tukisema watu wanatuchukia!! Hata kwa hayati Magufuli nilikuwa simuelewi kabisa kwa kuruhusu magari ya milioni 400 yanunuliwe na wakurugenzi wa halmashauri!! Hii Nchi bado tutapigwa sana!! Sijui wa kukomesha haya madudu atatokea lini ! Lakini naamini kama aliweza kutokea Magufuli basi yupo tu mwingine atatokea na atafanya Kweli kuliko hayati ! Atafanya yale yote mazuri na kwa weledi zaidi na hatofanya yote yaliyokuwa mabaya ambayo yalifanyika kipindi kile ! Mhe Mwigulu amenifurahisha kwa kuusema ukweli ! Kumbe wakosoaji hatustahili kulaumiwa kwa ukosoaji tunaoufanya ! Nchi hii inaliwa sana !!Ameongea ukweli mtupu
Unamaanisha estherNimemsoma mwigulu nimejikuta nacheka kwa masikitiko sana!
Amesahau gari analotumia kuwa nalo ni upigaji wa hali ya juu!
Aliaminisha watu kuwa watapunguza gharama za matumizi ya magari wiki ileile yeye akawa na gari la hali ya juu.
Acha watu wapige kwani nao wanataka kuwekeza ktk biashara ya magari ya abiria bwana.
Hakuna shughuli yeyote hapo ! Hiyo kazi inaweza ikadhibitiwa na mtu mmoja tu smart tena akiwa ameketi ofisini kwenye kiyoyozi ! Yeye ndiye atakuwa anaruhusu hicho kinunuliwe na kile kisinunuliwe! Leo dunia ipo kiganjani vipi iwe shughuli nzito ?! Ukiniambia peoples don’t give a damn of what’s going on hapo nitakuelewa!!Utekelezaji ndio shughuli nzito kwelikweli....
Hizo zinzopigwa si ni kodi?Nimemsoma mwigulu nimejikuta nacheka kwa masikitiko sana!
Amesahau gari analotumia kuwa nalo ni upigaji wa hali ya juu!
Aliaminisha watu kuwa watapunguza gharama za matumizi ya magari wiki ileile yeye akawa na gari la hali ya juu.
Acha watu wapige kwani nao wanataka kuwekeza ktk biashara ya magari ya abiria bwana.
Mbona bado pamoja na hayo vitu substandard vinanunuliwa?Utaratibu wa tenda unasababisha mtu anayetenda,kuingia gharama za ziada tofauti na utaratibu wa quatation. Hata iweje kama kitu kitanunuliwa kwa tenda bei yake itakuwa juu tu. Mfano yale makabrasha ya tenda wazabuni wanauziwa hiyo tayari ni gharama. Pili lazima walete dhamana ya benki nayo pia ni gharama tatu kuna document ya mwanasheria lazima waambatanishe hiyo nayo ni gharama, pia wanatakiwa wasupply kwanza bure ndipo baadae walipwe hivyo kama .mzigo ni wa mabilioni lazima wakope benki kwa kuchukua overdraft na baadae wakilipa wanalipa kwa riba. Pia mzabuni akishinda inabidi waingie mkataba hiyo mikataba nayo ni gharama. Hayo yote na mengine yanafanya bei ya kitu kinachonuuliwa kiwe juu kuliko ile bei unayoiona imebandikwa dukani. Nakubali kuwa bei elekezi ni muhimu lakini lazime izingatie gharama za ziada ambazo mzabuni anaingia vinginevyo litatengenezwa tatizo lingine la kununua vitu sub standard. Best way ni kununua moja kwa moja kiwandani kama vitu wanavyonunua ni vingi lakini sheria ya manunuzi inakataza kutokana na kipengele cha ushindani ambacbo kinasisitiza watu wasbindane.
Abanwe kwanza yeye mwenyewe ni mpigajiAmeongea ukweli mtupu
Matumizi yaanze na kubana bunge, haiwezekani budget ya miezi 12 inajadiliwa kwa miezi 3 ni utapeli na matumizi mabaya ya fedha za ummaWaziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuweka bei elekezi katika huduma na bidhaa inazonunua.
"Kwanini nchi nyingine za jirani na mashirika ya kimaitaifa wananunua magari kwa bei nafuu pengine zaidi ya nusu kuliko sisi serikalini" alihoji Nchemba.
"Haiwezekani hata kidogo lazima tukomeshe hali hii na tunaitegemea zaidi PPRA kutusaidia kutukwamua kutoka hapa ndani ya kipindi cha miezi michache katika mwaka huu wa fedha"alisema Mwigulu.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi Julai 15, 2022.