kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa. Njia pekee ya kubana matumizi ya serikali ni kwa kufanya yafuatayo:
1. Kuyafanya magari yote ya serikali yatumie gesi asilia badala ya mafuta na kuyafungia vifaa vya kuyafuatilia mienendo yao. Madereva wa magari ya serikali baadhi yao huwa wanaiba mafuta ya magari haya kwa kuyauza mitaani au kwa kudanganya kuwa wamejaza mafuta kwenye gari husika kumbe hawakujaza, wanashirikiana na wauza mafuta kwenye sheli.
2. Kupunguza idadi ya wabunge wasiokuwa na majimbo. Wabunge wote wote wawe wale waliochaguliwa na wananchi tu baaasi.
3. Kusimamia manunuzi ya umma kikamilifu
4. Kupunguza safari na misururu mirefu ya watu kwenye safari za viongozi wanaohitaji kugharamiwa.
5. Baraza dogo la mawaziri
6. Kupunguza gharama za chaguzi ndogo kujaza nafasi za wanaohamia, wanaojiuzulu au kufa kwa kumtangaza mgombea aliyeshindwa aliyekuwa na kura nyingi nyuma ya aliyekuwa ameshinda. Hii inaenda sambamba na kupima afya za wagombea kabla hawajapigiwa kura ili kujiridhisha na afya zao kabla ya kuchaguliwa.