The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,582
- 14,167
Atapeleka tuu kwani magari ya Wabunge huwa hayaendi Vijijini?H
Kuna wakati watu wanashindwa kutofautisha kati ya kusoma na elimu. Matumizi ya gari sio mafuta tu bro, bali kuna wear and tear za matairi, engine, break, oil, vioo, breakdowns, nk. Ni mjinga nani atakaependa kupeleka gari lake alilokopeshwa kwenda vijijini mbali, njia mbovu, matope kwenda kuhudumia jamii kwa gari lake binafsi? Ni nani atagharamia ununuzi wa matairi, spea na service ya gari ili ofisa aende safari za umma? Hii ni njia nyingine ya watumishi kuacha kwenda kuwahudumia wananchi kwa visingizio vya gari mbovu, matairi yamekwisha, gari inahitaji kufanyiwa service, nk.
Yaani niweke matairi yangu mapya kwenye gari langu halafu nitembelee kwenda kilomita 600 kwa kazi za serikali. Tutapunguza efficiency kwenye kuhudumia watu kwa kisingizio cha gari bovu.
Na kwa taarifa yako Serikali itakopesha magari yanayoweza kukabiliana na hayo mazingira.