Waziri Mwigulu: Kuna Bilioni 48 Wajasiriamali mtakopeshwa

Waziri Mwigulu: Kuna Bilioni 48 Wajasiriamali mtakopeshwa

mbongowakweli

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
848
Reaction score
684
Waziri Mwigulu asema ‘Wajasiriamali kuna Bilioni 48 mtakopeshwa’

c4a827b6-33da-4b07-b950-1cc7cac2ff31-860x573.jpeg
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema, kwa mwaka 2024, Mfuko wa Huduma Ndogo za Fedha – SELF unatarajia kutoa mikopo yenye masharti nafuu ya shilingi bilioni 48 kwa Wajasiriamali 48,000.

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mwaka 2024/2025, Bungeni Jijini Dodoma leo June 04,2024, Mwigulu amesema “ Mfuko huo unatarajia kukuza faida kabla ya kodi hadi shilingi bilioni 3.28 kutoka shilingi bilioni 1.89 mwaka 2023.

Kukuza mtaji hadi shilingi bilioni 65.48 kutoka shilingi bilioni 61.14 mwaka 2023” “Kuongeza idadi ya Wateja hadi 48,000 kutoka wateja 37,024 mwaka 2023, kukusanya marejesho ya mikopo iliyo nje ya mizania ya mfuko shilingi bilioni 2 na mikopo iliyo katika mizania shilingi bilioni 48.53 na kukusanya mapato ya jumla ya shilingi bilioni 11.03”
 
Kumbuka na yeye Ni mjasiriamali kwenye sekta ya usafirishaji, kubeti, sheli, mpira wa miguu n.k Sasa sio vibaya luxury zikaongezeka.
 
Kweli kabisa. Nilibahatika kumpata mama toka Mauritius, mwekezaji ZNZ na Bagamoyo. Aise wazembe wa SELF walimpotezea muda sijaona! Maombi mwezi wa nne, majibu mwezi wa nane!
Mwekezaji wa UTALII akazira! Akidai season ya utalii imekwisha hawezi zungusha huo mkopo!
Hao BOT, SELF, TADB ni JANGA KABISA! WAHUSIKA HAWANA HABARI, KAZI KUTUNGAZIA UMMA UPUUZI HUU...
 
TADB, SELF, MWIGULU, etc etc...
Zote kamba tu. Jaribu ku apply uone mlolongo, ucheleweshaji wa maombi, upotezaji muda, kujivuta vuta kwao, ubabaishaji, kutokuwajibika, uzembe na ufanyaji kazi wa mazoea ulivyokithiri!
HAMNA LOLOTE...
Daah pesa ni nyingi sana hila, ubabaifu ndio umekithili. Kila mmoja anatamani kuwa mnufaika wa fedha hizi, Hila zinaliwa tu na akina Mwigulu
 
Watapeana tu wenyewe, si mamayao alishawaruhusu wale kwa urefu wa kamba zao...ilimradi wasivimbiwe!.
 
Back
Top Bottom