Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Waziri wa Fedha amesema kuna matato ya Serikali yanaingia kwenye mifuko binafsi ya watu badala ya kwenda Serikalini.
Amesema kuwa hali hiyo hutokea kwenye ukadiriaji wa kodi au uuzaji wa bidhaa, amesema unakuta mtu anamwambia mteja nikupe bei ya Kupata na risiti au bei ya bila risiti?
Unakuta bei ya bila risiti ni ndogo kuliko ile ya risiti na hivyo kuwashawishi watu kutokulipa kodi. Anasema anayefanya hivyo anatenda kosa la uhujumu uchumi.
Amesema kwa watumishi wanaoshiriki kukosesha mapato serikali wanatenda kosa la uhujumu uchumi na kwamba hawatavumiliwa wala kuhamishwa kituo cha kazi bali wakibainika watafukuzwa kazi.
Ametoa wito kwa watu kutoa taarifa za watumishi hao wasio waaminifu na wala Watu wasipate hofu kuwa wakitoa taarifa watapata madhara kwa watu hao. Amesema watoe taarika kwa ofisi za TAKUKURU zilizo karibu.
Je, nini kifanyike ili kudhibiti watu wasiweke mifukoni mwao mapato ya Serikali? Toa maoni yako.