Waziri Mwigulu: Serikali imeomba msaada au mkopo wa trilioni 7

...Acha wakope bhana....hata hiyo Zanzibar ni sehemu ya Tz.
 
Ndugai alikufa kizembe tu kwa kushindwa kuisimamia hoja yake.
 
Na mlipaji ni mdanganyika
 
That is true.
 
Benki hazitoi misaada bali mikopo.
 
Mmeshampuuza ila sasa mnaanza kuwa na kigugumizi cha kuandika, mmeulizwa huo ni msaada au mkopo? jibuni.
Kama uko vizuri upstairs, ukiambiwa umepewa msaada na mkopo unaelewa nini?
 
Ukitoka huo mkopo ina maana ndani ya miezi 9 tutakua tumekopa 17trilion kama deni la nje. Hio trend unaona nzuri? Magufuli alikopa kwa akili na vitu alivyofanya vimeonekana.
Acha kujivua nguo mkuu, haya yote ni athari za Jiwe, japo ni ngumu sana kwa wewe kuelewa, jamaa ameleta maafa makubwa sana nchini. Ndiyo maana hata Mungu akaingilia kati kwani bila hivyo taifa kama taifa tungefika pabaya sana. Ukitaka kumjua vizuri Jiwe angalia watu wake wa karibu kama Bashite, Saambaya,Gamboshi, Ndungai, mzee wa jalalani na wengine wengi tu.
 
Kama uko vizuri upstairs, ukiambiwa umepewa msaada na mkopo unaelewa nini?

Naelewa mnajikanyaga mnajua kukopa sio kuzuri ndio maana mnatanguliza neno msaada kutupumbaza…
 

Athari za jiwe ni zipi…maafa yapi makubwa ameleta mkuu..tuelimishe huwenda watanzania wenzako tupo gizani
 
Unamuongelea Magu wa nini wakati hayupo na hawezi kujitetea? tumuongelee huyu aliyepo
Mkuu ndiyo maana wanasema tenda mema ukiwa hai ili ukisepa watu wakuongelee mazuri. Hata Nyerere mpaka leo anaongelewa, ishu ni kuwa unaongelewa kwa mabaya au mazuri. Jiwe alikuwa muuaji na muongo sana ndiyo maana anaongelewa kwa mabaya.
 
Mkopo na msaada???? Sasa hapo tumepewa nn mkopo, msaada au au vyote kwa pamoja
 
Athari za jiwe ni zipi…maafa yapi makubwa ameleta mkuu..tuelimishe huwenda watanzania wenzako tupo gizani
1:Watu wasiojulikana
2:Mauaji
3:Uongo
4:Wizi
5:Ukabila na ukanda
6:Utekwaji
Hayo ni machache, kama uko Tanzania basi waweza ongezea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…