Waziri Mwigulu: Serikali imeomba msaada au mkopo wa trilioni 7

Wakati washindani wa Tanzania kwenye biashara ya Logistics wakikopa kwa njia ya ku engage China Ili wajenge reli na miundombinu mingine ,huku Tanzania kuna Watu wenye akili mdogo hawataki.

Hata Kodi kulipa hawataki sasa unajiuliza Labda watapata maendeleo kwa kushushiwa na mvua.Ni hatari Sana kuwa na Nchi yenye Watu wenye akili kiduchu na mdomo mkubwa kama Tzn.

Matunda ya Ziara ya Foreign Minister wa China Kwenye baadhi ya Nchi za Africa.China imepanga kujenga reli ya sgr kutoka mpakani mwa Kenya/Uganda hadi Rwanda na DRC.

Kutoka Djibouti hadi Ethiopia ndani kabisaa.Watatumia model ya Belt and Road Initiative.

Ngoja Tzn tuendelee kujivuta na kubishana ujinga.





 
Hujajibu mkuu, nimekuuliza ukiambiwa umepewa mkopo na msaada unaelewa nini?

Nimejibu naelewa kwamba…mnatupumbaza kutumia neno msaada sababu kukopa manajua sio kuzuri..
 

Nimeshangaa mchumi hawezi kutofautisha mkopo na msaada, anaweka chachandu nyingii mara soft loan, mara masharti nafuu.

Jambo la kwanza kabisa atuambie ni msaada au mkopo? Hivyo ni vitu viwili tofauti japo vinahusiana kidogo.
 
Nimejibu naelewa kwamba…mnatupumbaza kutumia neno msaada sababu kukopa manajua sio kuzuri..
Aisee, hapo sina la ziada mkuu. Nikutakie asubuh njema kama uko nchi za Africa mana majira hatutofautiana sana japo si sawa.
 


Tutafaidika na nini mkuu kwenye huu mradi naomba utuelimishe watanzania wenzako
 
Mwigulu anajaribu kuepusha lawama, hizo pesa naamini ni za mkopo lakini kwasababu anajua walishaambiwa kukopa sio sifa wakamsuta aliewaambia, matokeo yake ndio haya anachanganya maneno "mkopo" na "msaada" kwenye sentensi moja.
hata ingekuwa ni msaada na sio mkopo bado ni tatizo, juzi Ndugai kasema na JPM aliwahi kusema hii misaada ni hela wanaitoa humu humu ndani, wanatufanya mazezeta wa kutupwa... worthless dunderheads
 
Ndani ya miezi 9 amevuka nusu ya deni la JPM la miaka 6…hili unaliongeleaje..
Kwani uongo wewe utakusaidia nini hasa? Serikali ya Samia imekopa 1.3 T na mara nyingi wamesema.

Mikopo mingine ilosainiwa na akina VC na Dotto James awamu ya 5 ila ilikuwa haijatolewa au inatolewa kwa mda fulani.

Ni kama hivi ambavyo Mwigulu kasaidi til.7 lakini zitatolewa over the course of 5 years to come.
 
Magufuli alikopa kwa akili!
Kukopa kwa akili maana yake nini?

Magufuli alikopa halafu akawa anaturubuni kila Jambo analolifanya ni kwa pesa zetu ilihali deni la taifa linakuwa

Kinachomgharimu mama ni uwazi si vinginevyo.
 
Ccm ni janga la kitaifa kauli ya spika aliyefurushwa itakuja kutimia muda sio mrefu
 
Hakuna asiekopa,ila kwa sasa habari za selikari zinazungumziwa zaid kuliko kipindi cha awamu iliopita,hii ni kwa sababu uhuru wa kuzungumza umekuwa huru sana,tofauti na hapo awali

Hapo awali kulikua na tozo? Tulikatwa kodi za lazima za jengo kwenye LUKU?

Kama kweli ni wa wazi watuambie makusanyo ya tozo na kodi za majengo zinakusanywa kiasi gani kila mwezi na zinatumika vipi.
 

Maafa kama yapi? Tuanzie hapa. Kupanda kwa gharama za maisha nako JPM anahusika? Acheni uchawa usio na faida uyo bibi yenu nchi imemshinda anatapatapa amekosa plan B. Muacheni mzee wa watu alale mmeona ndo wakumwangushia lawama lakini Watanzania wanajua umuhim wake.
 
Tutafaidika na nini mkuu kwenye huu mradi naomba utuelimishe watanzania wenzako
Reli tayari Mwendazake alishaanza kujenga na kama serikali ilivyosema washatumia til.14,,sasa kumtelekeza mradi huu ni kupoteza hizo til.14..

Busara ni kuumaliza na Kwa kuwa life span yake ni miaka 100 na zaidi inaweza wewe usifaidike wakafaidika wajukuu zako kesho..

Pili faida ya pesa moja kwa moja inaweza isipatikane but kama itachochea biashara hasa na Nchi jirani tayari hizo ni faida.nk nk.
 
Magufuli alikopa kwa akili!
Kukopa kwa akili maana yake nini?

Magufuli alikopa halafu akawa anaturubuni kila Jambo analolifanya ni kwa pesa zetu ilihali deni la taifa linakuwa.

Kinachomgharimu mama ni uwazi si vinginevyo.

Magufuli ameacha deni la sh. Ngapi? Na mbna waziri wa Fedha kipindi hicho alikua anatoa takwimu za deni la Taifa? Ukiona jambo linaongelewa sana ujue kuna shida- Akili mtu Wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…