Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Nchemba amesema kuwa mojawapo ya sababu zilizofanya wawakilishi wa nchi ( wabunge) waamue kukubali kupitishwa kwa tozo ni uwepo wa miradi mikubwa ya kimkakati inayoendelea nchini.
Ameyasema haya wakati akitolea ufafanuzi wa uwepo wa tozo nyingi zinazolalamikiwa na wananchi mtaani.
Ametolea mfano wa ujenzi wa Bwawa la Nyerere ambalo gharama yake inafikia kiasi cha trilioni 6, ujenzi wa reli ya kisasa, utoaji wa elimu bure pamoja na mikopo kwa wanafunzi.
Katikia kusisitiza hoja hii, waziri amesema kuwa hakuna nchi yoyote kwenye ukanda wa SADC inayoendesha miradi mikubwa yenye manufaa kwa wananchi kuzidi Tanzania.