Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 363
Nafikiri Takukuru na spidi walionayo sasa hivi watamwita Chiligati kwa Mahojiano innfact na Magufuli kwa ile tenda ya Samaki, halafu magufuli ilikuosha uso anasema mtakula samaki bure.Ndugu yangu Mtanzania,
Tanzania ni shamba la bibi, kila mtu akipata nafasi anavuna apendavyo. Swala la hizo gharama nilikuwa nime-reserve comments zangu na ndio maana nikasema tutaingia hasara mara 2.
Kama NHC ingekuwa inatengeneza faida ya mabilioni, ningeweza kuona kwamba it is worthy it, lakini wako choka mbaya. Hela za kujenga nyumba mpya hawana. Hela za kukarabati nyumba alizojenga Nyerere na zile tulizowadhulumu wahindi, hakuna. Leo Wizara inakwenda ku-spend shilingi milioni 70 kwa ajili ya kumpata MD/DG wa NHC!
Mimi ninafikiri kwamba Idara Kuu ya Utumishi wangeanzisha kitengo ambacho kingekuwa kina deal na kufanya recruitment ya watu kama hao badala ya kupoteza mamilioni ya fedha kwa kampuni binafsi. Tanesco nao wamefanya hivyo, lakini sijui wametumia fedha kiasi gani. Ni system nzuri inayosaidia kupata mtu mwenye sifa zinazotakiwa, but gharama zake zinakuwa inflated sana.
Ama watanzania tulio wengi ni mazezeta au tumerogwa. Hakuna mantiki usaili kutumika mapesa hayo nasi tunaendelea na maisha kama hakuna kilichotokea. Hivi mpaka litokee jambo gani ndio tuamke na kusema sasa basi? Hivi NHC shirika ambalo hata usimamizi wa nyumba zake unasuasua, utaratibu wa kumpata mkurugenzi mkuu nao unahitaji mihela mingi kiasi hicho? Hivi hawa jamaa nchi wanaipeleka wapi? Hata majibu yao ni ya kijeuri jeuri tu! Inaelekea tumeamua kusalimu amri na kukubali kuwa sasa tunatawaliwa na "ufalme" au "usultani" manake hawataki kuulizwa jambo lolote utadhani hii nchi ni mali yao! Itafika mahali tutalazimika kuwafyeka...Mungu apishie mbali.
*Inahusu zabuni ya kumpata bosi mpya NHC
*Alipuuza mapendekezo ya Ernst & Young
NA MWANDISHI WA RAIA MWEMA
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kapteni (mstaafu), John Chiligati, amejitumbukiza katika kashfa mpya ya kupuuza kazi iliyofanywa na Kampuni ya Kimataifa ya Ernst & Young iliyolipwa mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuendesha usaili wa kumpata Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), imeelezwa.
....
CHILIGATI: Nakwambia sikiliza bwana watu hawana shida ya kujua hayo yote, wewe nenda kaandike kwamba mchakato unaendelea na hivi karibuni na hasa mwanzoni mwa mwezi Novemba, mkurugenzi mkuu atatangazwa nitamtangaza mkurugenzi mkuu sawa?
....
Chiligati ana mtindo wa akili.Chiligati bwana,
Watu wana shida na kila sababu ya kuyajua yote haya. Hivi Kikwete ameacha kusoma raia mwema?
Acha jazba "waandishi" walimpigia simu na si kumfuata Dodoma.
Back to the mada, waziri sio rubber stamp awe anaidhinisha kila kitu tu, kama hajaji ridhisha anaweza kuachana na huo ushauri wa "kitaalam" vilevile, so tuliza ball kijana bongo tambarare!