Waziri mwinyi kijiuzulu hakukwepeki

The Infamous

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2009
Posts
731
Reaction score
121
Mimi kama Mtanzania nimeshidwa kuvumilia na mwendendo wa viongozi wa Serikali yangu yangu ya Tanzania kwa kutokuwa makini na kutoelewa nini maana ya uongozi, Maslahi ya mtu binafsi yamewekwa mbele kuliko Utanzania na kubebana bila kuwajibishana ndio suala lililopewa kipaumbele katika Serikali ya Mswahili. kwa mara nyingine tena Mbagala tumepoteza Watanzania watatu kwa uzembe wa watu wachache waliolewa madaraka na kuvaa viatu vya mkoloni..cha kusikitisha zaidi wanatoa vimilioni eti kuwafariji wafiwa, such a shame..mpaka sasa sielewi Waziri mwinyi amekaa kwenye hicho kiti cha uwazuri kwa ujasiri upi, na kauli zake 'kama ni uzembe ntajiuzuru' haya sasa wamekufa watatu tena tupe kauli nyingine..

kama muungwa na kiongozi adilifu TUNAOMBA JIUZURU kwani unatia hasira ila kama mtawala na mwenye moyo wa mimi ntakula wapi na familia yangu wacha wafe sikuzaliwa nao kaa kwenye madaraka.

POLENI SANA WAFIWA...
 
Yegho Masatu,

we huoni kosa hapo, kwanza Serikali na Jeshi walipishana ktk kutoa maelezo

Mmoja wanjeshi ndio waliotakiwa toa majibu kiufafanuzi zaidi kama Eneo la mbagala ni salama au hapana na wanajeshi walisema sio shwari na juzi wananchi waishio mbagala walisema kuwa wanajeshi walisema hapana usalama.

Serikali ikaingiza siasa zake hapo ati wananchi wasiwe na wasiwasi.

ivi kweli wanajeshi hawkupaswa kutupa tasmini ya kujua aina ya mabo hayo yaki ruka katika tukio la kwanza lilipotea yaweza kuwa yamenda umbali gani??

Mipango miji mibovu ktk eneo la mbagala iliwachukuwa muda gani wanjeshi wale wa kitengo maarumu wa kutegua mabomu na kutambua mabomu kumaliza kuyakusanya mabaki ya mabomu??

Hayo mambo yote yalifanywa kienyeji enyeji sana yani kwa muda mchache huo waliweza kukusanya mabaki na wananchi wakaruhusiwa kurejea majumbani kwao au kulikuwa na mkono wa mtu hapo??? watu walikwepa responsibility 100%

Kwaiyo Mwinyi kujiuzulu ilikuwa ni lazima ila viongozi wetu wanapenda mambo ya kudai hayo ni mipango ya Mungu till when tuwe twamsingizia Mungu kwa mauzembe yetu na kutokuwa wawajibikaji kwa wananchi wetu??
 
Infamous: Uko sahihi. Kujiuzuru mwinyi ni jambo ambalo liko wazi kama ingekuwa ni nchi za waliotangulia kustaarabika lakini kwa sababu ya utamaduni wa viongozi wetu hasa wa kiafrika, ataendelea kupeta tu huku watu wanazidi kupoteza maisha. Kinachouma zaidi ni kama ulivyosema kuwa watu wanapewa rambi rambi ya M1. Nafahamu hakuna soko la binadamu wala thamani yake kwa pesa lakini hizo rambi rambi jamani ziwe za kufuta machozi kweli.
 
mm cdhani km kujiuzulu kwa mwinyi ndio itakuwa suluhisho la tatizohili..mtoa hoja ulipaswa ujiulize kwanza kabla ya kuomba kujiuzulu kwamwinyi,, ulichopaswa kujiuliza ni kwamba(a)kambi ya mbagala na uwaziri wa mwinyi ninikilianza?('b)mabomu yalolipuka yaliwekwa wakatiwa uwaziri wake au ameyakuta?mm nadhani tatizo ni la muda mrefu,,, mipango miji yetu ni feki,,, kuweka pamoja kambi ya jeshi& makaz ya watu ni kitu kisichokubalika,,mwinyi ameikuta hali hiyo..la msingi ajitahidi kurekebisha kasoro zilizopo ili yalotokea yactokee tena...
 
Waziri Hussein Mwinyi mwenyewe alitamka kuwa iwapo itadhihilika kuwa uzembe ulisababisha ajali za Mbagala angejiuzulu; sasa mabomuyalilipuka na kuua watu na wataalam wanajeshi wakafanya kazi ya kukusanya mabaki ya mabomu toka uraiani. Katika kufanya kazi ya kukusanya masalia ya mabomu ,hawa wanajeshi walizembea nakuyaacha mengine ambayo juzi yameua watoto wengine; sasa kama huo si uzembe ni kitu gani? Kuna kila sababu ya waziri kujiuzuu ama sivyo nafsi yake itamuhukumu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…