Waziri Nape akabidhiwa uwanja wa uhuru uliojengwa na kampuni ya BCE Jijini Dar

sirluta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
6,325
Reaction score
2,491

WATANZANIA wametakiwa kuwatia moyo wachezaji wanaofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa kama,OLYMPIKI ambapo mwanariadha ALPHONSE FELIX SIMBU, alimaliza katika nafasi ya tano katika mbio za MARATHON mjini RIO nchini BRAZIL huku MKENYA ELIUD KIPCHOGE akimaliza wa kwanza na kunyakua medali ya dhahabu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari,utamaduni,sanaa na michezo NAPE NNAUYE baada ya kukagua uwanja wa uhuru jijini DSM ambao umejengwa na kampuni ya ujenzi kutoka china ya BEIJING CONSTRUCTION ENGINEARING GROUP BCE. Waziri NAPE pia amevitaka vyama vya Michezo hapa nchini,kujenga ofisi nje ya uwanja huo ilikuleta ufanisi wa utendaji kazi katika sekta hiyo

Katika jukwaa kuu la uwanja wa UHURU baada ya ukaguzi kukafanyika makabidhiano ya nyaraka za ujenzi wa uwanja huo ambapo katibu mkuu wa wizara ya habari,utamaduni,sanaa na michezo, PROF.ELISANTE OLE GABRIEL akawataka watanzania kuacha mara moja kuuita uwanja huu shamba la bibi.

Kwa upande wao mshauri mwelekezi wa uwanja huo, ALOIS PETER MUSHI na MENEJA MKUU KAMPUNI YA UJENZI BCE, PETER CHENG wamesema ujenzi wa uwanja huo umezingatia viwango vya kimataifa.

Waziri huyo pia amekangua mifumo ya matumizi ya tiketi za kielectroniki katika uwanja wa taifa ambapo zinategemewa kufungwa na kuanza kutumika SEPTEMBA NNE mwaka huu.

Chanzo: TBC
 
17 billions Tanzania shillings for rehabilitation only really?Kweli tunabana matumizi.
 
Watanzania siyo watunzaji wa vitu vyetu,kukamilika kwake ni hatua nzuri mno..
 
Walau tunaanza kuonekana tunafanya mambo makubwa hata kama wengine wataponda ila kikwetu tunasema " bilema olengile". Kuajaribu ni bora zaidi.
 
Its a good step,hopefully it will be well maintained.Its about time they do the same to other regional sports ground
 
Huo uwanja ungejengwa mkoa wa Pwani ingekuwa safi
 
Wasiusahau katika ile safari yao ya Dodoma waubebe.
 
Mbona sioni.uwanja wa maana apo...
 
Umepigwa viraka na kukarabati baadhi ya sehemu wala haujajengwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…