sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,491
WATANZANIA wametakiwa kuwatia moyo wachezaji wanaofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa kama,OLYMPIKI ambapo mwanariadha ALPHONSE FELIX SIMBU, alimaliza katika nafasi ya tano katika mbio za MARATHON mjini RIO nchini BRAZIL huku MKENYA ELIUD KIPCHOGE akimaliza wa kwanza na kunyakua medali ya dhahabu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari,utamaduni,sanaa na michezo NAPE NNAUYE baada ya kukagua uwanja wa uhuru jijini DSM ambao umejengwa na kampuni ya ujenzi kutoka china ya BEIJING CONSTRUCTION ENGINEARING GROUP BCE. Waziri NAPE pia amevitaka vyama vya Michezo hapa nchini,kujenga ofisi nje ya uwanja huo ilikuleta ufanisi wa utendaji kazi katika sekta hiyo
Katika jukwaa kuu la uwanja wa UHURU baada ya ukaguzi kukafanyika makabidhiano ya nyaraka za ujenzi wa uwanja huo ambapo katibu mkuu wa wizara ya habari,utamaduni,sanaa na michezo, PROF.ELISANTE OLE GABRIEL akawataka watanzania kuacha mara moja kuuita uwanja huu shamba la bibi.
Kwa upande wao mshauri mwelekezi wa uwanja huo, ALOIS PETER MUSHI na MENEJA MKUU KAMPUNI YA UJENZI BCE, PETER CHENG wamesema ujenzi wa uwanja huo umezingatia viwango vya kimataifa.
Waziri huyo pia amekangua mifumo ya matumizi ya tiketi za kielectroniki katika uwanja wa taifa ambapo zinategemewa kufungwa na kuanza kutumika SEPTEMBA NNE mwaka huu.
Chanzo: TBC